masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, April 19, 2014

CHASO KUUNGANA NA UKAWA KUWAELEZA WANANCHI JUU YA BUNGE MAALUM LA KATIBA



Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba


Jumuiya ya wanafunzi wa elimu ya juu Mkuo wa Iringa (CHASO) imeunga mkono tendo la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia bunge maalum la ktiba na kusema kuwa licha ya kufanyika hivyo limefanyika kwa kuchelewa.



Mtandao huu umeelezwa kuwa busara za wajumbe hao zimetumika kuliko kubaki kwenye vikao vya kudharirishana na kutukanana na kuacha kujadili maoni ya wananchi ambao wanatarajia kupata Katiba itakayosimamia haki zao na kusema kuwa watatumia nguvu zao kusaidiana na Ukawa kutoa elimu kwa wananchi.



Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Chaso Timotheo Mkanyia alisema hatua ya Ukawa imechukuliwa kwa busara na kwamba wananchi wanapaswa kuelewa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndio wanaovuruga mjadala wa vikao vya bunge maalum kutokana na vitendo vyao viovu vya kutumia matusi badala ya hoja.



Amesema dalili za bunge hilo kuvurugika zilianza kuonekana mapema kwenye hotuba ya mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa bunge hilo aliyoihutubia mjini Dodoma.



“Kauli za rais Kikwete ziliweka doa kwenye bunge hilo na isitoshe hakujua kama zinatia doa hata kwenye utendaji wake mwenyewe” amesema Mkanyia.



Amesema tatizo kubwa linalojitokeza ni kwamba mawaziri waliomo kwenye bunge maalum la Katika hawajielewi kuwa wao wapo pale kama wajumbe na si kwa kofia ya uwaziri au ubunge kwa kuwa lile ni bunge maalu na kwamba wanapaswa kuchangia kama wajumbe na si kwa kofia ya serikali.



Amesema wameshindwa kutumia ujumbe wao na kutumia madaraka yao vibaya na kusababisha vurugu na kukosa nidhamu katika bunge maalum la Katiba.



Amewatahadharisha wajumbe waliobaki kwenye bunge hilo kuwa kuendelea kudharau kilichoandikwa kwenye rasimu ni kuwadharau na kuwatukana wananchi ambao wametoa maoni hayo.



Amesema suala la Katima ni la maridhianao ambalo linahitaji kuheshimu mawazo ya kila mmoja na si wachache kuwadharau wengine.



Amewataka wajumbe wa Katiba kujua kuwa suala la kujadili rasimu ya Katiba ni kuboresha maoni yaliyomo na si kufuta kilichomo.



“Hoja ya serikali 2 ipo kwenye rasimu ipi na kwa maoni yaliyokusanywa wapi na kwa wakati gani?” amesema na kuhoji.



Amesema dhamira ya Ukawa ni ya dhati unaolenga kusimamia misingi na maslahi ya wananchi ambao walitoa maoni yakaandikwa kwenye rasimu hiyo.



Mkanyia amesema hoja ya makada wa CCM kuwa serikali tatu ni kuongeza gharama, ni hoja za kizushi na kwamba wanaosema hivyo wanapaswa kuwa na fikra pevu badala ya kuongea wasichokijua kwa kutaka kumridhisha mtu fulani.



“Kama suala la serikali tatu ni kuongeza gharama, nataka kuuliza je, mikoa inayoongezeka haina gharama za uendeshaji? Kama zipo zinatoka wapi na kwa maslahi ya nani?" amehoji.



“Tunashangaa kuona watu wanajikita katika serikali badala ya kufikiri ni namna gani watatatua matatizo yaliyopo kwenye huduma za kijamii” amesema.



Pia amesema serikali haipaswi kuzungumza chochote kuhusiana na rasimu ya Katiba kwa kuwa katiba inayotengenezwa ni ya wananchi na si ya viongozi wa serikali.



“Tume ya Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni kwa utaratibu uliowekwa kwa kuasikiliza wananchi wanachokitaka na si kwamba maoni yaliyomo kwenye rasimu hiyo ni ya kwake kama chama cha mapinduzi kinavyodai.



“Kumkejeli Jaji Warioba na kumtukana ni kuwakejeli na kuwatukanawananchi. Dhamira ya CCM ni kwamba wameona hali yao ni mbaya, wameshindwa kutimiza kile wananchi wanahitaji na kuona upinzani wana nafasi ya ushindi kuingia Ikulu kwa hiyo wanatanguliza hofu kwa wananchi ili waendelee kukumbatiwa na uovu wao” amesema.



Wamewataka Ukawa kufanya mikutno ya kutosha nchi nzima kuwaelimisha wananchi juu ya mwenendo mzima kwa bunge hilo jinsi lisivyozingatia demokrasia na utu.



“Tunaungana na Ukawa kutoa elimu kwa wananchi wajue jinsi wanavyotukanwa na CCM waliowasahau kuwa wao ni wapiga kura” amesema.



Katika hatua nyingine Chaso wamelaani vikali kauli za Waziri Lukuvi ambazo ni  za kichochezi kuwagawa watanzania katika ukabila na udini kuwa kiongozi huyo hakutumia busara.



Wamesema kauli za Lukuvi zinalenga kuliingiza Taifa pabaya kinyume na maoni ya wananchi wanaotaka kuishi kwa amani na kuwataka watanznia kutomkumbatia mtu anayewagawa kwa udini na ukabila.



Wamemta Rais Kikwete arejee hotuba yake ya uzinduzi wa bunge hilo kuwa ndicho chanzo cha matatizo ya kuingia katika machafuko.



“Rais akumbuke kuwa watu hawatamkumbuka kwa utawala wake bali watamkumbuka kwa mazuri, kuvuruga mawazo ya wananchi katika kutengeneza Katiba, ni kufuta mazuri aliyoyafanya. Tena kuunganisha kitu kimoja ukapata vitu viwili.



“TunawaasaWatanzania wote wenye nia njema na nchi yao tuungane kuhakikisha tunazishinda hila mbaya za CCM kwani tunaamini kuwa mfumo uliyopendekezwa kwenye Rasimu ndiyo suluhisho la kero za mda mrefu za Muungano” amesema.



Amesema Chaso ni waamini wa ukweli na hawatakwenda kinyume na kile wanachokiamini kwa kuwa ukweli ndicho chanzo cha mafanikio.

No comments:

Post a Comment