![]() |
| Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba. |
Jumuiya ya wanafunzi wa
elimu ya juu Mkuo wa Iringa (CHASO) imeunga mkono tendo la Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) kususia bunge maalum la ktiba na kusema kuwa licha ya
kufanyika hivyo limefanyika kwa kuchelewa.
Mtandao huu umeelezwa
kuwa busara za wajumbe hao zimetumika kuliko kubaki kwenye vikao vya
kudharirishana na kutukanana na kuacha kujadili maoni ya wananchi ambao
wanatarajia kupata Katiba itakayosimamia haki zao na kusema kuwa watatumia
nguvu zao kusaidiana na Ukawa kutoa elimu kwa wananchi.
Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Chaso Timotheo Mkanyia alisema hatua ya Ukawa
imechukuliwa kwa busara na kwamba wananchi wanapaswa kuelewa kuwa Chama cha
Mapinduzi (CCM) ndio wanaovuruga mjadala wa vikao vya bunge maalum kutokana na
vitendo vyao viovu vya kutumia matusi badala ya hoja.
Amesema dalili za bunge
hilo kuvurugika zilianza kuonekana mapema kwenye hotuba ya mwenyekiti wa chama
hicho Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa bunge hilo aliyoihutubia mjini
Dodoma.
“Kauli za rais Kikwete
ziliweka doa kwenye bunge hilo na isitoshe hakujua kama zinatia doa hata kwenye
utendaji wake mwenyewe” amesema Mkanyia.
Amesema tatizo kubwa
linalojitokeza ni kwamba mawaziri waliomo kwenye bunge maalum la Katika
hawajielewi kuwa wao wapo pale kama wajumbe na si kwa kofia ya uwaziri au
ubunge kwa kuwa lile ni bunge maalu na kwamba wanapaswa kuchangia kama wajumbe
na si kwa kofia ya serikali.
Amesema wameshindwa
kutumia ujumbe wao na kutumia madaraka yao vibaya na kusababisha vurugu na
kukosa nidhamu katika bunge maalum la Katiba.
Amewatahadharisha
wajumbe waliobaki kwenye bunge hilo kuwa kuendelea kudharau kilichoandikwa
kwenye rasimu ni kuwadharau na kuwatukana wananchi ambao wametoa maoni hayo.
Amesema suala la Katima
ni la maridhianao ambalo linahitaji kuheshimu mawazo ya kila mmoja na si
wachache kuwadharau wengine.
Amewataka wajumbe wa
Katiba kujua kuwa suala la kujadili rasimu ya Katiba ni kuboresha maoni
yaliyomo na si kufuta kilichomo.
“Hoja ya serikali 2 ipo
kwenye rasimu ipi na kwa maoni yaliyokusanywa wapi na kwa wakati gani?” amesema na kuhoji.
Amesema dhamira ya
Ukawa ni ya dhati unaolenga kusimamia misingi na maslahi ya wananchi ambao
walitoa maoni yakaandikwa kwenye rasimu hiyo.
Mkanyia amesema hoja ya
makada wa CCM kuwa serikali tatu ni kuongeza gharama, ni hoja za kizushi na
kwamba wanaosema hivyo wanapaswa kuwa na fikra pevu badala ya kuongea
wasichokijua kwa kutaka kumridhisha mtu fulani.
“Kama suala la serikali
tatu ni kuongeza gharama, nataka kuuliza je, mikoa inayoongezeka haina gharama
za uendeshaji? Kama zipo zinatoka wapi na kwa maslahi ya nani?" amehoji.
“Tunashangaa kuona watu
wanajikita katika serikali badala ya kufikiri ni namna gani watatatua matatizo
yaliyopo kwenye huduma za kijamii” amesema.
Pia amesema serikali
haipaswi kuzungumza chochote kuhusiana na rasimu ya Katiba kwa kuwa katiba
inayotengenezwa ni ya wananchi na si ya viongozi wa serikali.
“Tume ya Jaji Joseph
Warioba ilikusanya maoni kwa utaratibu uliowekwa kwa kuasikiliza wananchi
wanachokitaka na si kwamba maoni yaliyomo kwenye rasimu hiyo ni ya kwake kama
chama cha mapinduzi kinavyodai.
“Kumkejeli Jaji Warioba
na kumtukana ni kuwakejeli na kuwatukanawananchi. Dhamira ya CCM ni kwamba
wameona hali yao ni mbaya, wameshindwa kutimiza kile wananchi wanahitaji na
kuona upinzani wana nafasi ya ushindi kuingia Ikulu kwa hiyo wanatanguliza hofu
kwa wananchi ili waendelee kukumbatiwa na uovu wao” amesema.
Wamewataka Ukawa
kufanya mikutno ya kutosha nchi nzima kuwaelimisha wananchi juu ya mwenendo
mzima kwa bunge hilo jinsi lisivyozingatia demokrasia na utu.
“Tunaungana na Ukawa
kutoa elimu kwa wananchi wajue jinsi wanavyotukanwa na CCM waliowasahau kuwa
wao ni wapiga kura” amesema.
Katika hatua nyingine
Chaso wamelaani vikali kauli za Waziri Lukuvi ambazo ni za kichochezi kuwagawa watanzania katika
ukabila na udini kuwa kiongozi huyo hakutumia busara.
Wamesema kauli za
Lukuvi zinalenga kuliingiza Taifa pabaya kinyume na maoni ya wananchi wanaotaka
kuishi kwa amani na kuwataka watanznia kutomkumbatia mtu anayewagawa kwa udini
na ukabila.
Wamemta Rais Kikwete
arejee hotuba yake ya uzinduzi wa bunge hilo kuwa ndicho chanzo cha matatizo ya
kuingia katika machafuko.
“Rais akumbuke kuwa
watu hawatamkumbuka kwa utawala wake bali watamkumbuka kwa mazuri, kuvuruga
mawazo ya wananchi katika kutengeneza Katiba, ni kufuta mazuri aliyoyafanya.
Tena kuunganisha kitu kimoja ukapata vitu viwili.
“TunawaasaWatanzania wote wenye nia njema na
nchi yao tuungane kuhakikisha tunazishinda hila mbaya za CCM kwani tunaamini
kuwa mfumo uliyopendekezwa kwenye Rasimu ndiyo suluhisho la kero za mda mrefu
za Muungano” amesema.
Amesema Chaso ni waamini wa ukweli na hawatakwenda kinyume na kile
wanachokiamini kwa kuwa ukweli ndicho chanzo cha mafanikio.

No comments:
Post a Comment