![]() |
| Hati ya Muuungano wa Tanganyika na Zanzibar. |
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue alionesha hati halisi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyosainiwa na waasisi wa Muungano huo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume.
Hati hii inakuja maana ya mjadala mkuwa katika bunge maalum la Katiba juu ya kutokuwepo ama kuwepo kwa hati hiyo na kwmba iliyokwisha kuoneshwa si hati halisi.
Katika mjadala uliotawala katika kikao cha bunge maalum mjini Dodoma jana, Tundu Lissu alisema kuwa hati hiyo haipo jambo lililomlazimu Stivin Wassira kusimama na kuahidi kuwa angeiwasilisha bungeni humo baada ya siku 2.
Jioni ya jana ilimlazimu Katibu Kiongozi Sefue kuongea na vyombo vya habari ili kuweka bayana uwepo wa hati hiyo.
Wachambuzi wengi wanahoji kuwa kwa nini hati hiyo haikuonehshwa tangu mwanzo wa mjadala huo hadi wajumbe kukamiana ndipo uoneshwe?
Katika mjadala juu ya mwenendo a vikao vya bunge maalim la Katika uliofanyika kupitia kituo cha runinga cha Star Tv jana usiku, Edson Kamukara alihoji ni kwa nini hati hiyo ioneshwe sasa?
"Kwa nini sasa? Muda wote ilikuwa wapi? Nini kimefanya ioneshwe sasa?" alisema Kamukara.
Hata hivyo Kamukara alisema wajumbe wengi waliopo kwenye bunge maalumu, wamejikuta wapo pale kwa bahati mbaya kwa maana hawakupaswa kuwepo kutokana na kutokuwa na mchango wowote zaidi ya kupiga vigelegele na meza bila kujua wanachoshangilia.
Naye Gaudence Msuya kada wa chama cha Mapinduzi (CCM) alisema wajumbe waliopo kwenye mjadala wa uundwaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo pale kishabiki na kukiri kuwa na yeye ni muumini wa serikali mbili.

No comments:
Post a Comment