![]() |
| Meli ya Australia Ocean Shield iliyonasa ishara mpya |
Maafisa nchini Australia wanaongoza shughuli ya kuitafuta ndege ya Malaysia iliotoweka wamesema kuwa manuari moja ya wanamaji ya Australia imepata ishara zinazofanana na zile zinazotoka katika kijisanduku cheusi cha ndege chenye uwezo wa kurekodi.
Ishara hiyo imesikika katika kina cha takriban mita 4500 ndani ya bahari Hindi kupitia kwa chombo maalum kinachokokotwa na meli ya Ocean Shield .
Ishara hiyo ilinaswa na kurekodiwa kwa takriba Masaa mawili u nusu kabla ya kutoweka.
Afisa mkuu, Angus Houston amesema kuwa ni dalili nzuri zaidi kwao tangia shughuli ya kuitafuta ndege hiyo ianze.
Amesema kuwa Ishara hizo zilinaswa na meli moja kusini mwa bahari hindi yapata kilomita 1000 kutoka pwani ya Australia.
Lakini amesema kuwa uthibtisho kwamba ishara hizo zinatoka katika ndege hiyo ya Mh370 utachukua siku kadhaa kubainika.
Manuari nyengine ya Uchina Ilikuwa imeripoti kunasa ishara jumamosi iliyopita kutoka eneo tofauti ya Bahari Hindi.
![]() |
| Haixun 01 ya China Ilikuwa ya kwanza kunasa ishara |
Manuari hiyo Haixun 01, inasemekana ilikuwa ikitumia kifaa aina ya SoNar kunasa ishara hiyo iiliyodaiwa kuwa inarusha mawasiliano kupitia mitabendi 37.5 sawa na ndege kama iliyotoweka.
Madai hayo hayajadhibitishwa kufikia sasa japo meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Echo, imeelekea katika eneo hilo kutathmini chanzo cha ishara hiyo.
Chanzo: bbc swahili.


No comments:
Post a Comment