masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, April 30, 2014

ASKOFU: KUISHI KWA UADILIFU NA UAMINIFU NI KUUTAFUTA UTAKATIFU

Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akihubiri kanisani wakati wa maadhimisho ya Mika katika Seminari ya Mafinga.

Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwa pamoja na Mapadre na wanafunzi wa kidato cha sita wanaohitimu nje ya Kanisa mara baada ya Misa Takatifu.

Mhashamu askofu Ngalalekumtwa akikabidhi cheti cha mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita ukumbini.

Mhashamu askofu Ngalalekumtwa akihutubia wanafunzi na wageni waalikwa katika ukumbi wa Seminari ya Mafinga wakati wa mahafali.

RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka Wakristo nchini kuwa na hamu ya kumjua Mungu ili kustawisha Imani na kuishi katika mshikamano wa amani na upendo.

Askofu Ngalalekumtwa ameyazungumza hayo wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Seminari ya Mafinga katika Jmbo la Iringa na kusema kwamba kumjua Mungu ni kuishi katika uadilifu na uaminifu.

Amesema kazi ya kumtafuta Mungu ni wanadamu bali si Mungu kumtafuta mwanadamu kwani mwanadamu ameumbwa na kupewa akili na utashi wa kuweza kupambanua mambo mengi na kuchukua hatua ya maisha yanayompendeza Mungu au kuishi kadiri yeye atakavyo kwa maamuzi yake binafsi.

“Wakati tunaendelea kusherehekea Sikuu Kuu hizi za Pasaka tuwe na hamu ya kumjua Yesu Kama Tomaso alivyofanya. Imani ya Kipasaka ni ile inayoangazwa na Mungu Baba na Mwana na Kristo si wa kukimbizana naye bali ni wa kumkimbilia” amesema.

Amesema mwanadamu akiishi kwa haki atakuwa anatimiza maagizo ya Mungu anayetaka watu waishi bila kubughudhiana, waishi kwa upendo na kuacha chuki kwa kila mmoja.

Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa Jimbo la Iringa amesema uadilifu wa mtu humfanya kuheshimika na wengine na kwamba ndiyo njia ya kuufikia Utakatifu ambao Mungu anapenda wanaomtumainia waufikie.

“Uadilifu ni tunda ambalo tunalihitaji katika maisha yetu. Haki na uadilifu, haki na uaminifu ni tunda muhimu kwa wanadamu wanaompenda Mungu. Tunapaswa huishi kama viumbe wenye hekima” amesema.

Hata hivyo amesema Kanisa ndicho chombo cha kuandaa raia wa mbinguni ambao wanafundishwa kuishi kwa nidhamu wakiongozwa na kiongozi Mkuu Yesu Kristo.

Amesema kila mmoja anapaswa kumshika mwenzake katika umoja ambapo kila mmoja anayo mbegu ya utakatifu ambayo anatapaswa kupanda katika mioyo yaw engine kusudi waweze kuambukizwa utakatifu na hatimaye waweze kufuata maisha yanayompendeza Mungu na wanadamu hapa duniani na kuwa wanafunzi wazuri wa Yesu Kristo.

“Hakuna mnyonge ndani ya Kanisa kwani haki ni zile zile. Kuweni na utu na ubinadamu. Wote sisi ni watarajiwa wa mji wa mbinguni, kila mmoja ni mtakatifu mtarajiwa ila cha muhimu ni kuishi kwa haki. Tunaichezea huruma ya Mungu bila sababu.

“Waakatifu Yohane wa XXIII na Yohane Paulo wa II ni watu wa kuigwa katika maisha yetu. Katika kutangazwa watakatifu hawa watumishi wa Mungu, unakumbushwa kuwa ni watu wa amani, upendo, huruma na tunapaswa kuishi kama viumbe wenye hekima” amesema.

Misa hiyo ilikwenda sambamba na mahafali ya kidato cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 41 waliagwa katika Seminari hiyo.

Akiwakabidhi vyeti wanafunzi hao, askofu Ngalalekumtwa amewataka kutumia elimu yao katika kuunganisha watu kuishi maisha ya kupendana na kuepukana na mambo yasiyo na maana ambayo ni chanzo cha kuvuruga amani na upendo.


Amewataka kuwa viongozi wa mfano kwa ulimwengu kwa uishi katika maisha yenye kuzingatia haki za binadamu na kuwa kioo kwa kila wakubwa kwa wadogo.

No comments:

Post a Comment