| Waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa wakielekea Mtaa wa Ilala kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani hii leo. |
| Waandishi wa Habai wa Mkoa wa Iringa wakifanya usafi katika Mtaa wa Ilaa Siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya Habari duniani. |
WAKAZI wa Mtaa wa Ilala katika Manispaa ya Iringa wamesusa
kufanya usafi katika mtaa wao kwa kile walichoeleza kuwa wanachangishwa
michango kwa ajili ya usafi.
Madai hayo yamekuja baada ya waandishi wa Habari kukusanyika
kufanya usafi mtaani humo katika siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya
Habari duniani.
Wakiohijiwa na mtandao huu mtaani humo, wakazi wa mtaa huo
wamsema ofisa mtendaji wa mtaa pamoja na ofisa mtendaji wa Kata ya Ilala
wamekuwa wakichukua mchango kwa wananchi kwa ajili ya usafi lakini hakuna
kinachoendelea.
Wakieeleza kuto kujitokeza kuungana na waandishi wa habai
walikua wakifanya usafi katika mtaa wao, wamesema wasingejitokeza kutokana na
tabia ya viongozi wao kuwahadaa kuchukua fedha pasipokufanya kazi yoyote.
Alipotakiwa kutaoa ufafanuzi juu ya suala hilo, ofisa afya
Kata ya Ilala Gaudence Haule amesema
kutokujitokeza kwa wananchi kunatokana na watendaji wa mitaa kutoa taarifa
sahihi kwa wananchi juu ya kushiriki usafi katika mtaa wao.
“Taarifa walizopewa wananchi kwa watendaji wao juu ya
kushiriki usafi siyo sahihindiyo maana waandishi mnaona wananchi hawana hata
mpango wa kushiriki licha ya kuwa mnafanya usafi katika maeneo yao wenyewe.
“Suala la uafi ni la mtu mmoja mmoja kuanzia kwake mwenyewe
lakini inapofikia mtu hawajibiki hata sehemu yake mwenyewe usafi wake binafsi
unatia shaka. Tusipobadilika hakika itakuwa ngumu hata kwetu wenyewe juu ya
afya zetu” amesema.
Wakati huo huo Katibu Mtendaji wa Chama cha waaqndishi wa Habari
Mkoa wa Iringa Francis Godwin amesema
licha ya Manispaa ya Iringa kuwa ya pili kwa usafi kitaifa, bado inakabiliwa na
changamoto kubwa juu ya usafi kwa ujumla kutoka na wananchi wewenyewe kutokuwa
na mwamko wa ufasi.
Amemtaka ofisa usafishaji wa Manispaa kuhakikisha vitendea
kazi vinakuwepo kila eneo ili wananhi waweze kuwajibika kufanya usafi ipasavyo
badala ya kutupa taka hovyo kila sehemu.
Godwin amesema waandishi
wa Habari Mkoa wa Iringa wameamua kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari kwa vitendo ili kuuonesha umma vyanzo mbalimbali vya Habari ikiwa ni
pamoja na sehemu zao wanazotupa taka.
Pia amesema waandishi wa Habari kufanya usafi, ni kuionesha
jamii kuwa mwandishi anawajibika kwa mwananchi katika mambo mbalimbali
yanayomzunguka katika maeneo yake.
Ofisa usafishaji wa Manispaa Alon Mafumiko amesema suala la
usafi katika Manispaa ya Iringa linakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ya
wananchi kuchoma vifaa vya kuhifadhia taka na kwamba kati mapipa ya taka 50
yaliyokua yamesambazwa na Manispa katika Manispaa nzima kwa ajili ya kubebea
taka yamechomwa na wananchi na kubaki mapipa 10 tu.
“Nawaomba wanachi watambue kuwa sehemu bila usafi siyo
ustaarabu kwa hiyo kila mmoja awajabike ili tuweke mazingira yetu safi” amesema
Mafumiko.
No comments:
Post a Comment