masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, April 29, 2014

WAFANYAKAZI ZA STRABAG WAGOMA KWA KUBAGULIWA

WAFANYAKAZI wa Kampuni inayojihusisha  na  ujenzi wa barabara ya  mradi wa mabasi  yaendayo haraka (BRT)  ya Strabag, jana wamegoma kufanya kazi kutokana na kubaguliwa katika malipo  ya stahili  na posho.

Akizungumza  na mtandao huu  jijini Dar es Salaam  jana kwa niaba ya wafanyakazi wenzake, Mwenyekiti  wa Chama cha Wafanyakazi  Strabag, Abdullah Rukusa, alisema  sababu kubwa ya mgomo huo  ni ubaguzi  unofanywa na uongozi wa juu katika suala la malipo ya stahili  zao ya sh 65,000 za  wafanyakazi hao.

Rukusa alisema wafanyakazi wa kampuni hiyo hasa wazawa wamekuwa wakibaguliwa katika malipo na kwamba raia wa kigeni  wamekuwa wakipewa  kipaumbele.

Alisema ingawa kesi ya madai yao ipo mahakamani, lakini wanashangazwa na utaratibu uliopo ambao unawafanya kufanya kazi katika mazingira magumu, jambo ambalo linazorotesha na kuchelewesha umalizikaji wa  Barabara ya Morogoro.

“Tunabaguliwa sana, haiwezekani raia wa kigeni walipwe posho na stahili zao sisi Waafrika tusilipwe.

Tunataka haki itendeke katika suala zima la malipo, vinginevyo wote tusitishiwe  malipo,” alisisitiza.

Meneja Uajiri wa Strabag, Nelson Mlumba, alisema hawezi kuzungumza lolote kwa kuwa wanaingia kwenye kikao ambacho kitakuja na majibu na suluhisho la matatizo ya wafanyakazi wao.

Chanzo: Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment