WATUMISHI wa Mungu wametakiwa kuzingatia maadili yao katika
maisha yao yote kwa kuishi kwa tabia njema ili waeze kushiriki kazi ya kulea na
kuwalisha wanadamu maneno ya kiroho.
Wamekumbushwa hayo leo na mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
wa Jimbo la Iringa alipokuwa akitoa daraja Takatifu la Ushemasi katika Kanisa
Kuu la Kiaskofu Parokia ya Kihesa jimboni humo.
Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania na msimamizi wa kiti cha kitume Jimbo Kuu la Songea amesema huduma
ya shemasi inaambatana na maisha ya useja ambapo wanapaswa kuelekezamiili yao
kwa Mungu.
“Mashemasi wanapaswa kuwa na tabia njema ili waweze kuishika
siri ya imani katika dhamiri safi. Miili yao, mioyo yao na nafsi yao yote imuelekee
Mungu kwa umoja usiogawanyika” amesema.
Amesema mashemasi ni walezi ambao wanapaswa kuwamfano
wakuigwa bila kupenda kupita njia za kijanja kwa kujificha bali wanapaswa
kufanya kazi zao kwa uwazi.
Amefafanua kuwa huduma ya mashemasisi katika Kanisa Katoliki
ni kuwa msaada kwa askofu na Baba Mtakatifu ili waweze kuhudumia altare,
kuongoza sala, kusimamia na kubariki ndoa, kuongoza sala, kuongoza ibada ya
mazishi na kuwahudumia wanadamu wote kwa upendo.
Pia amesema Mashemasi wanashiriki kutangaza habari njema kwa mataifa
ili jamii yote iweze kuishi kwaupendo thabiti na kukemea mambo maovu
yanayohatarisha amani ya wanadamu kote duniani kwa kuwa Kristo hupenda amani.
Hata hivyo anawakumbusha kuwa wao ni watunzaji wa siri ya
wokovu na watendaji katika kuwapeleka wanadamu kwa Mungu.
“Iweni na moyo wa huruma, upendo kwa watu mnaowahudumia. Tunzeni
nafsi zenu ili msilaumiwe mnapohudumia. Kuanzia sasa mtakalokuwa mnalitenda
mnalitenda kwa niaba ya Kanisa Katoliki.
“Jitahidini kutenda kwa haki na usafi siyo kwa ujanja ujanja.
Kuweni wajumbe wazuri katika kutoa huduma njema. Kuweni naheshima, uaminifu,
upendo, nidhamu, utiifu, upole na uadilifu wa Kristo ili mkaitende kazi iliyo
haki kwa watu wote” amesema.
Pia amewataka Wakristo kuwaombea watumishi waMungu ili
katikahudumazao wapewe nguvu ya kumshinda mwovu shetani na kufanya haki kila
wakati.
No comments:
Post a Comment