![]() |
| Wapiganaji wa Boko Haram |
![]() |
| Watu waliohama makwao mjini Maiduguri |
Wapiganaji wa Kiislamu nchini NIgeria wamekishambulia kijiji Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo na kuwaua kiasi ya watu 18.
Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumapili katika kijiji cha Alau Ngawo katika jimbo la Borno.
Mkuu mpya wa jeshi Nigeria, Alex Badeh ametoa wito wa kumalizwa haraka kwa mashambulio hayo.
Rais Goodluck Jonathan alitangaja hali ya hatari
katika majimbo matatu ya eneo hilo, likiwemo Borno, mnamo mwezi Mei
mwaka jana, lakini kundi la Boko Haram limekuwa likiendelea kufanya
mashambulio
Watu hao waliouawa na wanamgambo wa Kiislamu wamezikwa katika kijiji kimoja Kaskazini Magharibi mwa Nigeria, siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa ulinzi wavamia hao walishambulia kijiji hicho na kuteketeza maakazi yao.
Wamama kadhaa na watoto wameripotiwa kujeruhiwa
vibaya wakati wa shambulio hilo, lililofanywa na watu waliokuwa
wamejihami kwa bundi na kusafirishwa kwa magari na piki piki huku
wakiimba Mungu ni mkubwa walati walipokuwa wakiyapora makaazi ya watu
ili kuiba mali na Chakula.
Jeshi la Nigeria Limeshindwa?
''Baadhi yetu ambao tulisikia wakiwasili mapema,
tulifanikiwa kutoroka, lakini baadhi ya wenzetu ambao walikuwa wamelala
hawakufanikiwa kutoroka kabla ya wanamgambo hao kuwakamata'' Alisema
mwana kijiji mwingine.
Madai hayo ya raia huyo yamewuiana na yale ya afisa mwingine wa ulinzi ambaye hakutaka kutajwa.
Wakaazi wa kijiji hicho cha Alau, iliyoko katika
mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri kwanza walizika miiili ya
wakulima kumi na sabaa, kabla ya kupata mengine mawili.
Shambulio hilo limetokea kufuatia shambulio
katika vijiji vya mpakani, ambako nyumba kadhaa ziliteketezwa na raia
kuuawa na wapiganaji hao wa Boko Haram.
Watu kumi na watano waliuawa kwenye shambulio
hilo wiki iliyopita katika kijiji cha Gashigar, mashambulio ambayo
yaliwalazimisha raia wengi wa Nigeria kutorokea nchi jirani ya Niger.
Wiki iliyopita rais wa Nigeria Goodluch Jonathan alitangaza mabadiliko makubwa katika uongozi wa jeshi la nchi hiyo.
Maafisa wote wakuu waandamizi walifutwa kazi na
afisa wa jeshi la anga kutoka eneo hilo linalokabiliwa na mzozo wa
Kaskazini Mashariki aliteuliwa kuwa kamanda mpya wa Jeshi.
Chanzo: bbc swahili


No comments:
Post a Comment