| Mgombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Oscar Ndale akiwa kwenye gari akiwapungia wananchi mkono wakati wakitoka kuhani msiba kabla ya kuanza mkutano Ukumbi. |
| Patrick Ole Sosopi akiwahutubia wananchi wa Ukumbi. |
| Brian Kikotiakiwahutubia wananchi wa Kata ya Kukumbi jana. |
| Katibu wa Mbunge wa Ubumbo (Chadema) akiwahutubia wananchi wa Ukumbi. |
| Mbunge wa viti maalumu Chiku Abwao (Chadema) akiwahutubia wananchi wa Ukumbi jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za kumnadi mgombea kupitia chama hicho. |
| Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao kushoto akimnadi mgombea wa udiwani Oscar Ndale kulia na nyuma ni Brian Kikoti wakiwa jukuani. |
| Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao (Chadema) akiwa na viongozi mbalimbali wachama hicho. |
| Kada wa Chama cha Mapinduzi God Mbilinyi aliyenusurika kichapo kwenye mkutano wa Chadema jana Ukumbi. |
| Mwananchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wakimsikilizamgombea wa udiwani wa Chadema katika Kata ya Ukumbi jana. |
| Watu mbali mbali wakiwa kwenye mkutano wa Chadema jana katika Kata ya Ukumbi. |
UZINDUZI wa kampeni za kumnadi mgombea wa wa udiwani kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Kata ya Ukumbi Wilaya ya
Kilolo mkoani Iringa jana ulitaka kuingia dosari baada ya kijana anayeaminika
kuwa ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Gody Mbilinyi kunusurika kichapo.
Mbilinyi alinusurika
kichapo na wananchi waliokuwepo kwenye mkutano huo kwa madai kuwa ametumwa na
CCM kuleta fujo hali iliyowalazimu Brian Kikoti na Mbunge wa viti maalum Chiku
Abwao kumnusuru kuwa aachwe.
Hali hiyo ilijitokeza
wakati Kikoti akiwa jukuani akinadi sera na kumnadi mgombea wa Oscar Ndale pale
Mbilinyi alipotokea nyuma ya pale walipokuwa wamekaa viongozi wa Chadema ambapo
mayowe yalianza akamatwe huyo huku wakianza kumsogelea jambo lililomlazimu
Kikoti na Mbunge Abwao kusimama na kuwataka aachwe.
“Mmwacheni huyo hata
kama ametumwa hakuna jambo baya tunalolifanya hapa. Mkutano wetu ni wa amani
upo kwa mjibu wa sheria, hatujaja kutukana kama walivyofanya wao jana hapa
kuporomosha matusi badala ya kunadi serazao. Sisi tutakuwa wa mwisho kujibu
mapigo kwa sababu tupo makini” alisema Kikoti.
Akimuombea kura mgombea
wa Chadema alisema CCM wamekuwa ni watu wa ahadi zisizotekelezeka ambapo kila
siku wanaeleza ahadi tu na kusahau kuwa walikwisha kuahidi kitu hicho hicho
ikashindikana kutekeleza.
“Ukumbi sasa tumechoka
kuletewa mamluki. Sasa tunataka kijana mwenye upeo, mwenye uchungu na
wanaukumbi wenzake, ambaye anaonja machungu moja kwa moja. Si mtu wa kuja”
alisema.
Patrick Ole Sosopi
alisema umefika wakati wa kuachana na watu wanaowageuza wenzao kuwa mitaji yao
huku maisha yakiwa mabaya kila kukicha.
“Tukiendelea kukubali
wanavyotudanganya tutakuwa wajinga. Zaidi ya miaka 50 tumekuwa na maadui watatu
maradhi, ujinga na umasikini na sasa ameongezeka adui mwingine ambaye ni rushwa
inayosababishwa na CCM.
“Kilolo ina rasilimali
nyingi ambazo zinatakiwa kumsaidia kila mmoja lakini badala yake kumekuwa na
michango inayokuwa kero kwa wananchi. Hatuhitaji michango inayowabughudhi watu
bali tuataka michago inayoleta maendeleo” alisema.
Akimnadi mgombea
kupitia Chadema Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao (Chadema) alisema mapenzi ya
CCM kwa wananchi yamekwisha na kuwataka wanaukumbi kutumia nafasi iliyopo
kuikataa.
Alisema ukombozi wa
wananchi upo katika uwezo wao na kwamba kitendo cha Ukumbi kuwakatika sura
inavyoonekana sasa kwa muda wa zaidi ya miaka 50 ni adhabu.
“Kitendo cha kuwanyima
elimu watu wa Kilolo si cha bahati mbaya. Sura mliyo nayo watu wa Kilolo si
sura halali. CCM wamewazidi ujanja wanawaibia waziwazi, viongozi wengi
mnaowachagua hawana nia njema na nyie.
“CCM mnayoiona leo si ile ya Mwalimu Nyerere. Heshima
ya CCM ilikwisha wakati wa kifo cha hayati Mwalimu Nyerere ambaye alisimamia
haki kwa kila mmoja. Viongozi wa CCM waliopo sasa ni walafi tu hawana huruma na
wananchi wao” alisema.
Naye mbombea wa udiwani
kupitia chama hicho Oscar Ndale alisema pindi atakapopata nafasi kwa wananchi
ya kuwawakilisha atahakikisha miradi yoteiliyopo ndani ya Kata ya Ukumbi
anaisimamia kwa umakini ili iwaletee manufaa wananchi.
Alisema atapambana na wale
wote wanaotumia rasilimali za umma kwa ubinafsi na kurudisha heshima ya Kata
ambayo ina kila utajiri.
“Wamegeuza Ukumbi kuwa
ni mtaji wao. Naomba kura zenu ili nikapambane nao huko huko kuhakikisha haki
yetu tunaipata. Kodi tunalipa lakini hatuoni faida yake kumbe wapo wachache
wanaojinufaisha kupitia kodi zetu. Nitawabana ipasavyo ili tuheshimiane”
alisema Ndale.
Licha ya kuwa katika
uzinduzi huo kulikuwa na mvua, wananchi walikomaa kusimama kwenye mvua hadi
mwisho wa mkutano.
No comments:
Post a Comment