RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, askofu wa Jimbo la Iringa na Msimamizi wa kitume Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa anawaagiza waamini wote Tanzania kuanza Sala za kuliombea Bunge la Katiba ili wajumbe wafanye mjadala kwa amani, haki, uadilifu na umakini ili Katiba itakayopatikana iwe ya haki na manufaa kwa watanzania wote.
Amesema hayo alipokuwa akiongea na mtandao huu ofisini kwake leo kwa kutaka waamini wote watambue kuwa kazi inayofanywa na wajumbe ni ya Taifa.
Amesema Sala ni nguzo ya amani, haki na umoja na kwamba wajumbe wa Katiba wakitanguliwa na Roho Mtakatifu na kufanya mjadala kwa hofu ya Mungu watafanya haki kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Amewataka waamini wote kuanza sala za kuliombea Bunge hilo kila wakati ili kusiwe na kikwazo chochote na hatimaye waweze kuitengeneza Katiba yenye manufaa itakayoleta maendeleo kwa watu wote.


No comments:
Post a Comment