| Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake leo. |
| Waandishi wa habari wakimsikiliza meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ofisini kwake leo. |
MAMLAKA ya Mapato (TRA) Mkoa wa
Iringa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wafanyabiashara
waliosajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani kutokutumia ipasavyo mashine
za kielekitroniki za kutolea risiti.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake leo, Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda alisema
wapo baadhi ya wafanyuabiashara wasiowaadilifu ambao hawatumii mashine za
kutolea risiti ipasavyi na kuiingizia serikali hasara.
Ametaja changamoto nyingine kuwa
ni pamoja na kutotoa na kudai risiti wakati wa kuuza na kununua bidhaa au
huduma mbalimbali.
“Pia kuna changamoto nyingine
ambazo zinatokana na kuingia kwa bidhaa zilizopigwa marufuku kama vipodozi,
pombe aina ya “power one”, double puch na bidhaa nyingine kama sukari kuingizwa
hapa nchini kwa njia za magendo pamoja na mwitikio mdogo wa wafanyabiashara wa
kununua na kutumia mashine za kielektroniki” amesema Mwenda.
Amesema wanafuatilia kwa ukaribu
matumizi ya mashine za kielekitroniki za kutolea risiti kwa wafanyabiashara
wote waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani na kuhakikisha wanazitumia
vilivyo, kuzuia ukwepaji wa kodi katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa
kutokutoa risiti wakati wa kuuza na kwa ununua bidhaa au huduma mbalimbali
pamoja na kuzuia bidhaa zilizopigwa marufuku zisiingizwe nchini kwa njia za
magendo.
“Tumejipanga kukuza na kusimamia
maadili mema ya wafanyabiashara katika kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na
taratibu za ajira na kuendelea kutkeleza mpango mkakati wa miaka mitano wa nne
ulioanza 2013/2014 na na ambao utafikia mwisho wake 2017/2018” amesema.
Amesema katika utekelezaji wa
mipango hiyo ni kujenga uwajibikaji wa hiari na wa hali ya juu wa kulipa kodi
ambapo ambapo mamlaka lazima ijenge uwezo mkubwa wa kusimamia sheria za kodi,
uwezo wa kudhibiti ukwepaji kodi na utendaji unaozingatia uadilifu wa hali ya
juu wa wafanyabiashara wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Mamlaka ya Mapato Tanzania
imeanza kuadhimisha siku ya mlipa kodi Novemba 2 ambapo kilele chake
kinatarajiwa kufikia Novemba 8 Mwaka huu.
Katika maadhimisho ambayo ni ya
saba tangu kuanzishwa kwake Oktoba 2006, ni kutambua mchango wa walipakodi na
kuwatunuku walipakodi ambao wapo mstari wa mbele katika kuweka kumbukumbu zao
za biashara kwa usahihi, wanaolipa kodi zinazolingana na biashara zao,
wanaojituma kulipa kodi kwa muda unaostahili kisheria na wale wanaolipa kodi
zao kwa hiari ambapo jumla ya wafanyabiashara 24 watatunukiwa vyeti kwa kufanya
biashara zao kiutaalam.
Mwenda amesema katika maadhimisho
hayo ambayo kaulimbiu yake ni “tulipe kodi kwa matokeo makubwa sasa”
yataisaidia jamii umuhimu wa ulipaji kodi kwa matokeo makubwa, kupata mrejesho kutoka kwa
walipakodi na wateja wengine kwa ujumla kama juu ya huduma zitolewazo na
mamlaka hiyo zinaridhisha na kwamba zina ubora pamoja na kuwakumbusha
walipakodi haki na wajibu wao katika ulipaji wa kodi.
Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa
kwa mwaka wa fedha 2012/2013 imekusanya jumla ya shilingi 29,271,160,861.55
sawa na asilimia tisini (90%) ya utendaji ikiwa walipangiwa kukusanya jumla ya
shilingi 32,650,500,000.00/=.
Lengo la Idara ya Ushuru wa
Forodha lilikuwa shilingi 302,500,000/= na lengo la Idara ya Kodi za Ndani
lilikuwa shilingi 32,348,000,0000/= ambapo kwa makusanyo hayo ya zaidi ya 29
Bilioni yaliyokusanywa, yanaonesha ukuaji wa mapato ya shilingi 4,540,408,676
ukilinganisha na makusanyo ya shilingi 24,730,752,185.00 ya mwaka 2011/2012.
Kuelekea kilele cha maadhimisho
ya siku ya mlipakodi kitakachofanyika Novemba 8, mwaka huu kitakachofanyika
katika ukumbi wa Highlands , Mamlaka ya Mapato
Mkoa wa Iringa imetoa msaada wa shilingi 700,000/= katika kituo cha kulelea
watoto yatima cha Daily Bread Life.
Kipindi cha miaka 16 iliyopita
TRA Mkoa wa Iringa imekuwa ikipanda na kushuka katika ukusanyaji kodi kutokana
na changamoto mbalimbali.
Hata hivyo takwimu zinaonesha
katika kipindi hicho, jumla ya watu 6,665 walitembelea ofisi za TRA kwa masuala
ya yanayohusu kodi.
Licha ya changangamoto
zinazoikabili Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha miaka 16 iliyopita
ukusanywaji wa kodi umebainishwa ambapo mwaka huu (2012/2013 unaonekana
kutekelezwa kwa asilimia 90 tofauti na kwaka 2011/2012 uliotekelezwa kwa
asilimia 105.
Mwaka 2010/2011 ukusanywaji wa
kodi ulitekelezwa kwa asilimia 87 chini ya mwaka 2009/2010 uliotekelezwa kwa
asilimia 105, mwaka 2008/2009 ulitekelezwa kwa asilimia 110 wakati mwaka
2007/2008 ulitekelezwa kwa asilimia 106.
Mwaka 2006/2007 ulitekelezwa kwa
asilimia 139 wakati mwaka 2005/2006 ulitekelezwa kwa asilimia 103 ambapo mwaka
2004/2005 ulitekelezwa kwa asilimia 107 wakati mwaka 2003/2004 ulitekelezwa kwa
asilimia 102.
Mwaka 2002/2003 ulitekelezwa kwa
asilimia 102 huku mwaka 2001/2002 ukitekelezwa kwa asilimia 104, mwaka
2000/2001 ukitekelezwa kwa asilimia 83, mwaka 1999/2000 ulitekelezwa kwa
asilimia 86 na mwaka 1998/1999 ukitekelezwa kwa asilimia 112, mwaka 1997/1998
ulitekelezwa kwa asilimia 106.
No comments:
Post a Comment