masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, October 2, 2013

MSISHABIKIE MAMBO MACHAFU NA NJIA HARAMU KUJIPATIA MAFANIKIO: ASKOFU


BINADAMU amekuwa mshabikiaji wa mambo kwa lengo la kujipatia mafanikio hata kama njia anazozitumia ni chafu hali inayopofusha maisha ya utakatifu.

Haya yamezungumzwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Tosamaganga katika jimbo la Iringa ikiwa ni maadhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu.

Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa na mlezi wa jimbo Kuu la Songea amesema binadamu wa leo wamekuwa wagumu kushauriwa na kuonywa kwa kuwa wanatumia njia chafu kujipatia utajiri.

Amesema kiburi kimetawala na kusababisha haki za watu kupuuzwa huku wachache wakinufaika kwa kupitia njia haramu jambo lililo kinyume na mpango wa Mungu.

“Tunashabikia kile tunachoona kitatuletea raha. Tunashabikia ili kufikia malengo yetu hata kama ni kwa njia haramu. Tunashabikia majina makubwa, fedha, vyeo hali inayopofusha maisha na maisha yetu ya utakatifu” amesema Ngalalekumtwa.

Amesema mwisho wa hayo yote ni machungu na majuto yasiyoisha kwani ni ukaidi wa makusudi kuendekeza kiburi badala ya upole na unyenyekevu ili kufuata njia sahihi.

Amesema mwanadamu anapoonywa na kukemewa kwa kile anachokifanya kinyume cha utaratibu na makubaliano ya jamii au jumuiya ameona kama ananyanyaswa na kuwa na majigambo na kiburi kukaidi onyo analopata hata ka kama ni kwa faida yake mwenyewe.

“Asituambie mtu kitu, asituonye au kutukemea, jibu lake ni unyanyasaji na kujenga kiburi kuishi katika ukengeufu, tumekuwa na majigambo na kiburi, hatutaki kuambiwa kitu na mtu yeyote na hata sauti ya Mungu tumeizibia masikio” amesema.

Amesema kila mmoja anapaswa kujiuliza kama anaishi katika haki na uadilifu kwa kushirikiana na wengine katika katika kuwatendea wengine matendo mema.

Amesema kuishi vizuri hapa duniani ni kutengeneza histori na kumbukumbu ambayo itaigwa na wengi kama watakatifu walivyofanya katika maisha yao.

Hata hivyo amesema binadamu ameteuliwa na Mungu ili aweze kuishi katika haki na uadilifu kwa kuwajali wale wote wanaohitaji kupata huduma na msaada.

“Tumeteuliwa na Mungu kuishi katika haki na uadilifu. Sisi walimwengu wa leo tunajiwekea malengo ambayo tunaamini yatashibisha mahitaji yetu na tumeshindwa kupekua neno la Mungu lakini mambo mengine tuna muda.

“Uteuzi huo unatutaka kufanya kile Mungu anataka tufanye na kuishi katika maisha mazuri yenye Baraka katika kuwatumikia wanadamu wenzetu” amesema.

Amesema maisha ya mwanadamu yamekuwa ni ya ubabaishaji na kufanya mambo hovyo bila kujali hukumu anayoweza kupata kutoka kwa Mungu.

Amesema Imani ndiyo inayompa mtu ujasiri wa wa kutetea haki na wajibu wake kwa kumtumikia Mungu na wanadamu wenzake katika uadilifu na ustahimilifu.

“Tujenge urafiki na watakatifu maana wao wana hamu nasi. Watakatifu ni washenga wetu, ni daraja linalotupeleka uzimani. Swali la kujiuliza ni kwamba, tunaishi katika haki? Tukiishi vizuri hapa duniani, tutakumbukwa kwa matendo yetu” amesema.

Amewataka wakristo kuwa na tamaa ya kufika mbinguni waliko watakatifu na malaika wanaotamani binadamu kufika huko waliko kwa kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

“Watakatifu wanatamani sisi tuishi vizuri, tuishi vema ili tuweze kuufikia utakatifu huko mbinguni” amesema.

Pia amesema binadamu wawe na ujasiri wa kutetea na kusimamia imani zao na uinjilishaji kwa ajili ya kusaidi roho za watu ziweze kupata wokovu na kuufikia uzima wa milele.

“Kuweni n a ujasiri wa kutetea Imani na uinjilishaji ili roho za wanadamu zipate kufunguliwa na kuenenda katika Kristo” amesema.

Wakatoliki pia wameashwa kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya kujenga familia ya Mungu yenye upendo na amani kwa kuishi katika mshikamano na umoja.

Amesema magumu yanayotokea isiwe sababu ya mwanadamu kumuacha Mungu na kukimbilia njia zisizo halali katika kutafuta suluhu bali Kristo pekee ndiyo jibu la kila jambo na kwamba mwanadamu anakabiliwa na changamoto kubwa ya kupambana na vishawishi vinavyorudisha Imani na kukatisha tamaa ya kumtafuta Mungu.

Amesema kila mtu anapaswa kuwa na hekima, busara, kuwa mpole na mnyenyekevu kwa ili kuwa na mahusiano mazuri na wenzake kwa ajili ya kulinda na kudumisha amani ya taifa ili jamii iweze kuishi kwa furaha kila wakati.

“Roho wa Mungu atawale kila sehemu maana yeye ni roho wa hekima, upendo, upole, ushuhuda na ukarimu. Tuishi katika hayo ili tuweze kuongezwa thawabu kubwa ya maisha hapa duniani na kujiongezea hazina ya uzima huko mbinguni” amesema.

Amesema kuishi maisha ya utakatifu kunahitaji moyo wa kujitoa na kuacha mambo mengine ambayo ni ya anasa na kuacha kupenda kufanya mambo kwa njia zisizo halali kwa kutaka kupata mafanikio ya haraka.

“Sisi wanakanisa tujawe na moyo wa kujitoa, moyo wa huruma, ukarimu ili tuwasaidie wahitaji wote. Tuendelee kuishi katika upendo aliotuachia Kristo kwa ajili ya utukufu wake. Tusiwe na chokochoko za kuvuruga amani. Tulinde imani yetu katu katika hali ya utulivu na heshima tukimtukuza Mungu wengu aliye juu” amesema.

Amesema kejeli kwa watu wengine zisifanyike na badala yake kila mmoja atumie nafasi yake katika kumuomba Mungu.

Amesema wakristo watumie muda wao kutangaza injili kupenyeza kwenye mioyo ya watu ili hata wale wasiomfahamu Kristo waweze kumtambua na kumfuata.

“Kwa maombezi ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, tuwe na moyo wa ukarimu ili Kanisa lijieneze, lipenye mioyo ya watu. Kwa maombezi ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu, Mungu awalinde na kuwatunza ili mdumu katika  moyo wa shukrani” amesema.

No comments:

Post a Comment