masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, October 3, 2013

"HATUTASITA KUJILINDA NA KULINDA BENDERA ZETU KAMA VITENDO HIVI VITAENDELEA": MBUNGE MSIGWA

Mgunge wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) aliyevaa kofia akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ya Chadema Wilaya na kulia kwake ni Katibu wa chama hicho Wilaya Suzan Mgonukulima.

Diwani wa Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi (CHADEMA) akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ya Chadema Wilaya na kulia kwake ni Katibu wa Wilaya Chadema Suzan Mgonukulima.

MBUNGE wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) amekemea vikali vitendo vya kupiga wananchi na kung’oa bendera za Chadema vinavyofanywa na vijana wa Chama cha Mapinduzi (Green guard) wakati wa ukimbizaji wa bendera ya chama hicho na picha ya Rais Kikwete.

Msigwa ametoa rai kwa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa kutofumbia macho vitendo hivyo na badala yake waongeze ulinzi ili kuepusha vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Amesema kuijiunga na chama ni hiari ambapo kila mtu yupo huru kuchagua chama anachopenda kujiunga na kwamba siasa chafu zinazofanywa na CCM ni zisifumbiwe macho kwani ni chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani.

Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ya Chadema Wilaya leo, Msigwa amesema kukaa kimya hakumaanishi kuwa Chadema imeshindwa la kufanya ila ni ustaarabu tu ambao wameamua kuufanya ili kutoa nafasi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuthibiti vitendo hivyo.

“Mimi napenda kuwaasa ndugu zetu wa chama cha mapinduzi kuwa tufanye siasa za ustaarabu. Kila wanakokwenda wakikimbiza bendera na picha wanapiga watu. Huo ni utarataibu gani? Tusingependa kujibu kwa vitendo hivyo wanavyovifanya bali tunaomba wajirekebishe” amesema.

Amesema vijana wanaotumika na chama cha mapinduzi kupiga watu na kung’oa bendera za Chadema waache mara moja vitendo hivyo bila kulazimishwa.

Amesema vitendo vinavyofanywa na vijana hao huku viongozi wao wakikaa kimya vinaamaanisha ni mipango mikakati walio nayo katika chama kufanya fujo kwa watanzania wasio na hatia.

“Uwezo wa kujirudishia tunao lakini tumeamua kunyamaza kimya si kwa sababu tunawaogopa bali ni ustaarabu tu. Ila vitendo hivi vikiendelea hatutasita kujilinda na kulinda bendera zetu ambazo zinaharibiwa bila sababu” amesema.

Wakati wa ukimbizaji wa bendera katika halmashauri ya Iringa, vijana wa CCM walipiga watu katika vjijiji vya Ifunda na Ihemi jana wakati Nduli na Isimani nako watu wakipigwa kwa madai kuwa wamevaa nembo za Chadema huku wakiong’oa bendera za Chadema katika Wilaya ya Kilolo ambapo mwenyekiti wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kilolo Sifuni Makongwa akituhumiwa kuratibu mpango huo.

Makongwa alikamatwa katika Kata ya Ilole aking’oa bendera za Chadema jambo alilolazimika kuomba msamaha kwa vijana waliokerwa na vitendo hivyo na kuachiwa huku akiahidi kuwa atalipa gharama za bendea hizo.

Sambamba na hilo Msigwa amesema michango ya Mwenge inayoendelea mjini hapa ni ya wizi kwa kuwa haina tija yoyote kwa wananchi na kuwataka wananchi wasilazimishwe kutoa mchngo bali waamue wenyewe.

“Mwenge hauna tija yoyote; wananchi msilazimishwe kutoa mchango huo kwa sababu kuna watu wamejitengenezea ulaji. Tumieni hela zenu katika shughuli za msingi, changieni shughuli za maana tu. Si kwamba tunakataa michango lakini mchango wa Mwenge hauna maana. Tutasimama na kuvalia njuga pale tunapoona kuna tija ili wananchi tuchangie lakini michango isiyo na maana hatutaki iwaumize.

“Na ieleweke kuwa shughuli za kuchangia au kutokuchangia siyo za wanasiasa bali ni za viongozi serikalini. Ipo michango inayohidhinishwa na serikali Kuu na ipo michango ambayo watu wachache wanaianzisha kwa maslahi yao wenyewe. Epukeni michango ya unafiki kwa kuwa itawaumiza” amesema.

Hivi karibuni wafanyakazi wa taasisi mbalimbali katika Manispaa ya Iringa na halmashauri ya Kilolo wamelalamika vikali juu ya michango ya Mwenge wanayolazimishwa kuchangia.

Pamoja na malalamiko hayo, wameeleza kuwa japo kuwa kila mwaka huchangia, kwa mwaka huu imekuwa tishio kwa kutakiwa kuchangia sare kwa shilingi elfu 25 huku mchango wa Mwenge Pekee ukiwa ni shilingi 1,000/=.

Vyanzo vyetu mbalimbali vimeeleza kuwa kuna kiongozi ambaye amebuni kufanya biashara hiyo na kushawishi wakuu wa idara kupitisha ili waweze kuwakamua wafanyakazi kinguvu  huku wakijua kuwa kipato chao bado hakikidhi mahitaji.

Taarifa zinasema kuwa wapo baadhi ya wakuu wa idara ambao wamekuwa wakitumika kwa ajili ya kuwaumiza wafanyakazai wenzao kwa kutaka kusifiwa na kupandishwa vyeo jambo ambalo limekuwa likiwaumiza wafanya kwa kiwango kikubwa.

Wakati wafanyakazi waliopo ndani ya Manispaa ya wakilalamika na kulaani, wafanyakazi waliopo ndani ya Halmashaur ya Kilolo wamesikitishwa na kitendo cha kukatwa mshahara kwa madai ni michango ya Mwenge.

Vyanzo mbalimbali kutoka Kilolo vimeeleza kuwa wafanyakazi hawakushirikishwa juu ya michango hiyo lakini wameshangazwa kuona mshahara wao ukiwa pungufu.

“Watu wana mambo ya ajabu kweli, wamekata mshahara lakini tulipokwenda kuhoji mishahara imekatwa kwa sababu gani eti wanatwambia michango ya Mwenge! Mbona huu ni unyonyaji mkubwa sana? Watu wanatumia mwenge kuiba mishahara ya watu.

“Tukiendelea kwa mtindo huu sijui tutafika wapi! Mbona nchi hii imekuwa kama ya watu waigizaji wasio na ubinadamu? Mwalimu atakumbukwa kwa mengi” kilisema chanzo chetu.

Wakati wafanyakazi wa Manispaa wakitakiwa kuchanga kiasi cha shilingi 26,000/= kwa ajili ya Mwenge, wafanyakazi wa Kilolo wamekatwa 10,000/= katika mishahara yao kila mmoja.

Hata hivyo mtandao huu umefanikiwa kunasa barua ambayo imeandikwa na kusambazwa kwenye taasisi mbalimbali na kusainiwa na Christina Nyato kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa yenye Kumbukumbu namba IME/E.10/34/VOL.IV/27 kuwata watumishi kutoa michango hiyo.


Oktoba 14 mwaka huu Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzimwa kitaifa katika Mkoa wa Iringa.

No comments:

Post a Comment