masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, September 26, 2013

MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIMALA AMKATAA MWENYEKITI WA KAMATI YA SHULE


MWALIMU Mkuu wa shule ya msingi Kimala Kata ya Kimala Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa Ahamed Twalipo, amemkataa mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo huku akitoa vitisho kutumia ushirikina kummaliza.

Twalipo ametoa vitisho hivyo baada ya mwenyekiti wa kamati ya shule Telaki Ndenga kuitisha kikao cha kamati hiyo ili kujadili  namna gani wanaweza kukabiliana na matatizo ya shule hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo.

“Kamwe sitafanya kazi na mwenyekiti wa kamati ya shule. Anachonifuatilia mimi nini nini?” alisema.

Kinasa sauti cha Tanzania Daima kilifanikiwa kunasa sauti ya vitisho ambayo mwalimu huyo aliitoa kwa mwenyekiti huyo na kusababisah wjumbe kubaki midomo wazi.

“Kama ni mpango wako mimi nifukuzwe kazi au nihamishwe, Kimala sihami ng’oo wala haachishwi kazi mtu hapa. Labda niwe sikuaga nyumbani.

“Unafikiri hata nikishushwa cheo au niachishwe kazi wewe utakuwa mwalimu mkuu? Mtu mwenyewe hujasoma halafu unaleta usumbufu kwa tuliosoma. Mbumbumbu mkubwa we! Kimala utakatika Mnyororo tu, hakuna wakuning’oa” alisema Twalipo.

Kikao kilianza kuvurugika mapema kabla ya kuanza baada ya Mwalimu Mkuu wa shule kumsukumia mwenyekiti manano ya kashfa kuwa hatashirikiana naye kamwe kwa kuwa hajasoma.

Mwalimu huyo aligeuka kuwa mbogo na kusababisha wajumbe waliokuwa wamekusanyika kufanya kikao hicho kutojua cha kufanya jambo lililowalazimu kuvunja kikao na kutoa agizo kwa mwalimu huyo kuitisha mkutano utakaomshirikisha mratibu wa elimu ili atoe maneno hayo mbele yake.

“Kimala hii nitadili na watu watatu nikianza na Telaki Ndenga huyu mwenyekiti w kamati ya shule, Like Mbwelwa na Boniface Kasuga kwani hawa ndio wanaonifuatilia mimi. Ama zangu ama zao nitadili nao hadi mwisho” alisema.

Akijibu kauli za mwalimu huyo, Telaki Ndenga mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo alisema anashukuru kwa hatua alipofikia mwalimu huyo na kwamba majibu yote yatapatikana ndani ya kamati ya shule na si penginepo kama anavyofikiri mwalimu huyo.

“Hata akitumia vitisho kuwa yeye aliaga nyumbani kwao, majibu yatapatikana hapahapa wala hayatatoka nyumbani kwao kama anavyosema kwa kuwa shule hii ni yetu si ya familia yake” alisema Ndenga.

Kukataliwa na kutishwa kwa mwenyekiti wa kamati ya shule kunakuja wiki chache baada ya gazeti hili kuchapisha tuhuma anazokabiliwa nazo mwalimu mkuu katika shule hiyo ikiwemo ya kuanzisha michango kwa kila mwanafunzi kiasi cha shilingi 47,000/= elfu wakiwemo watoto yatima.

Awali wananchi walitoa malalamiko yao kuwa mwalimu huyo amekuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na vitisho kwa wazazi wanaofika shuleni hapo kutaka ufafanuzi wa uhalali wa michango hiyo na mara nyingine kuwadharirisha wazazi mbele ya watoto wao shuleni hapo.

Mwalimu Twalipo anadaiwa kuuza chakula walichochanga wananchi kwa ajili ya wanafunzi wawapo shuleni hapo mchana kwa madai ya kukarabati nyumba za walimu bila kushirikisha kamati ya shule.

No comments:

Post a Comment