| Banda linalotumika kuabudia Kigango cha Luganga Parokia ya Kilolo jimbo la Iringa. |
| Kamati ya ujenzi wa Kanisa iliyoteuliwa ikiongozwa na Francis Mwilafi. |
| Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania akimtambulisha Francis Mwilafi (aliyefunika uso) mwenyekiti wa ujenzi wa Kanisa mara baada ya kuteulliwa. |
| Francis Mwilafi mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa Kanisa akiongea mara baada ya ukuteuliwa. |
“KUWA kiongozi serikalini au kwenye chama fulani haimaanishi
kuwa upo mbali na Mungu, kinachotakiwa ni kutumia nafasi katika haki”.
Haya yamezungumzwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania
Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa akihubiri katika Kanisa la Kigango
cha Luganga Parokia ya Kilolo katika jimbo la Iringa na kwamba kiongozi bora ni
yule anayefanya kazi kwa hofu ya Mungu na kutenda haki kwa binadamu wenzake.
Amesema maisha yanayompendeza Mungu ni kwenda kinyume n a ufisadi
na kuepukana na mambo ya hovyo ambayo ni kikwazo kwa wanadamu wengine.
“Usiwe kiongozi mbabaishaji, tapeli, fisadi au mdanganyifu.
Kila mmoja anatakiwa kuwa mwaminifu katika nafasi yake. Wewe ni kiongozi katika
serikali au chama, timiza wajibu wako” amesema.
Mhashamu askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni skofu wa jimbo
la Iringa na msimamizi wa jimboa la Songea amesema ulinzi wa mali za taifa
umetoweka kutokana na watu waroho, wenye uchu wa mali wanaopenda wwengine
kuishi kama watumwa.
“Kuna watu wana uchu na rasilimali za taifa letu na
kutufanya wengine kuishi maisha ya umasikini wa kutupa. Tuwajibike katika
wajibu zetu ; linda mali za taifa lako, misitu, ardhi, gesi, petrol na wanyama
ili vitumike kwa manufaa ya taifa zima badala ya watu wachache” amesema.
Amesema binadamu amekuwa akitumia muda mwingi kusaka na
kufukuzia mali na kumsahau Mungu japo kuwa Mungu amemjalia mwanadamu mtaji wa
akili na utashi ambavyo anashindwa kuvifanyia kazi kwa umakini.
Amewataka wakristo kutumia akili kuishi na watu ili
kuwafanya wengine kuishi kwa furaha ambayo ndiyo maagizo ya Mungu.
Amesema uzuri wa maisha ni kuishi kwa kumpendeza Mungu kwa
kuwahurumia wengine na kutoa haki sawasawa na mapaswa ya binadamu na mahitaji
yake.
“Hata kama wewe ni kiongozi wa kisiasa au serikalini, wekeza
katika haki. Tutendeane vizuri kwa haki wala tusiburutane kwa kigezo cha mali”
amesema.
Hata hivyo amewaasa wakristo kuishi kwa amani na kutokuwa na
moyo wa kisasi bali kuishi katika kuvumiliana na kushauriana ili kumfanya kila
mmoja kuishi kwa amani.
Amesema msingi imara wa maisha ya mkristo ni upendo, huruma,
amani, msamaha, upole, unyenyekevu na utii ambavyo ndivyo vinajenga maisha ya
kuishi na watu wengine kama familia.
Pia amesema mkristo anapaswa kuishi kwa kwa moyo wa kujitoa
katika masuala mbalimbali ya kijamii nay a kiroho na kuwa mfano mzuri wa kuigwa
katika maisha yasyo kikwazo kwa wengine bila kuingiza itikadi za chuki,
ubaguzi, ubinafsi, masengenyo na dhuruma.
Amesema binadamu wa leo wamekuwa kigeugeu wasio na mwelekeo
kwani wengi wao wametanguliza maslahi yao binafsi na uroho wa mali hata
kudiriki kunyang’anya haki za watu kwa manufaa yao.
Amesema Mungu amemuumba mtu kwa makusudi lakini binadamu
amegeuka kuwa adui wa wengine kwa kuishi kama mnyama mkali asiyetakiwa
kusogelewa.
Amewataka watanzania kwa ujumla kutokubali kuusa ardhi yao
kwa watu na badala yake waitumie vizuri kwa ajili ya matumizi na maendeleo ya
vizazi vijavyo.
“Tumieni ardhi kwa maendeleo yenu wenyewe. Msiuze ardhi kwa
kumaliza shida ya siku moja. Watu wanafanya udanganyifu kwa kutaka ardhi huku
wakiwaacha wengine kukosa mahali ambapo wanaweza wakafanya maendeleo. Hiyo ni
dhambi kubwa” amesema.
Misa hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa michango ya
ujenzi wa Kanisa jipya ambapo jumla ya shilingi 1,672,250/= zilipatikana pap0
hapo huku ahadi zikifikia shilingi 2,730,000/=, mifuko ya cement 15, kuku 1 na
tofali 1,600.
Kanisa jipya litakalojengwa linatarajia kubeba watu zaidi ya
900 ambapo ujenzi wake unatarajia kuanza mapema.
Ili kuhakikisha ujenzi huo unakuwa na usimamizi makini,
Francis Mwilafi ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ambayo ina
jumbla ya watu 7.
Akizungumza mara baada ya kuteuliwa, Mwilafi amesema atahakikisha
shughuli za ujenzi huo zinakuwa mfano na kwamba kila kila anayeguswa kuchangia
milango iko wazi.
No comments:
Post a Comment