masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, August 5, 2013

UTEJA WETU KWA WANASIASA WAONGO BASI: WANAWAKE

George Abwao akikabithi fedha kwa mhasibu wa kikundi cha wanawake cha "Chiku Abwao" ili ziweze kugawiwa kwa kufanyia biashara ndogo.

Chajia Baya katibu wa kikundi cha wanawake akihesabu fedha hizo baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya kuanza kuzigawa.

George Abwao pamoja na viongozi wakihakiki hesabu ya fedha zilizogawiwa kwa wananwake wa kikundi hicho.

Wanawake wakicheza kufurahia fedha walizopata kwa ajili ya kufanyia biashara.

WANAWAKE wamesema uteja wao na wanasiasa wanafiki na waongo wanaowatumia kama viwanja vya mpira umekwisha baada ya kugundua mbinu zao chafu wanazozifanya.

Wakizungumza jana wakati wa kupeana mkopo katika kikundi walichokiita “Chikua Abwao” kilichopo katika Mtaa wa Kinegamgosi “A” Kata ya Ruaha katika Manispaa ya Iringa wamesema kwa miaka mingi wanasiasa waongo wamekuwa wakiwatumia kama viwanja vya mpira kwa kutoa ahadi zisizotekelezeka huku wakigawa vitenge na kofia wakati wakiomba kura na baada ya hapo wanatelekezwa.

Katibu wa kikundi hicho Chajia Baya alisema Mbunge Chiku Abwao (CHADEMA) ni wa aina yake kwa kuwa hana propaganda na ni mtu asiyependa kuahidi uongo na badala yake amekuwa ni mtu wa utekelezaji wa moja kwa moja bila kuchelewa.

“Mbunge wetu Chiku Abwao ni wa pekee, ni mtu asiyetumia jukwa kwa kuahidi uongo bali anakwenda moja kwa moja katika utekelezaji. Wiki lililopita tulikaa naye tukaunda kikundi hiki leo hii amekwisha kutekeleza kile alichoahidi. Wapo wanasiasa wengi ambao kila unapokaribia uchaguzi wanaanza kutudanganya sisi akina mama na kibaya zaidi hata wanawake wenzetu wametugeuza sisi kama maroboti. Uteja wetu kwao umekwisha.

“Wanaotambua matatizo yetu ndiyo wanaojitoa ili watuwezeshe kutukomboa kuondokana na umasikini tulio nao. Umasikini wetu unatokana na watu wanaotaka kutumia nafasi hiyo kutudanganya ili tuwachague. Sasa wadanganyifu hao waige mfano wa mwanamke mwenzao Chiku Abwa (Mbunge viti maalum) kwa kile anachokifanya kwa wanawake wenzake” alisema.

Hata hivyo alisema wapo baadhi ya watu wanaojitokeza kuunda vikundi vya wanawake kwa madai ya kuwasaidia wanawake wenzao na baada ya kukusanya fedha za wanawake hao wanatokomea kusikojulikana.

Akikabidhi fedha za mkopo kwa mhazini wa kikundi hicho kwa niaba ya Mbunge huyo, George Abwao ambaye ni mume wa Mbunge huyo alisema nia kubwa ni kuleta maendeleo kwa wanawake ili waweze kuinuka kiuchumi badala ya kubaki wakiburuzwa na wenye fedha.

“Tunachotaka ni maendeleo tu. Hatuna maneno mengi ambayo si ya msingi ila tunachowaomba akina mama, jitahidini kuzitumia fedha hizi kwa ajili ya maendeleo na kurejesha kwa wakati ili kila mwanakikundi anufaike” alisema Abwao.

Alisema uaminifu na uajibikaji ni jambo muhimu katika maendeleo na kuwataka akina mama hao wasisikilize maneno ya uongo wanayoambiwa na watu wasiopenda maendeleo na badala yake watumie muda wao kwa ajili ya kufanya maendeleo.


Jumla ya shilingi 655,000/= zimetolewa kwa akina mama hao ili waweze kufanya biashara ndogo kwa ajili ya kusaidia kuinua kipato chao na kuziinua familia zao.

No comments:

Post a Comment