![]() |
| Rwasa alitoroka Burundi baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 akihofia maisha yake |
Kiongozi wa zamani wa
upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa anarejea nyumbani baada ya miaka mitatu
ya kuwa nje ya nchi.
Rwasa alikua kiongozi
wa chama cha FNL lakini alipokonywa uongozi baada ya kutoroka nchi akihofia
maisha yake.
Mwanasiasa huyo
aliondoka Burundi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, alipolalamikia kwamba
uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.
Umoja
wa Mataifa umekua ukiwasihi wanasiasa wa Burundi waliokimbia nchi, kurejea
nyumbani kama hatua ya kuondoa taharuki za kisiasa.
Hata
hivyo serikali ya Pierre Nkurunzinza imekuwa ikimuona Rwasa kama tisho la
kisiasa tangu kutoroka nchi hiyo, ingawa Rwasa alirejea mjini Bujumbura kwa
shangwe na vigelegele kutoka kwa wafuasi wake baada ya kuhakikishiwa usalama
wake.
Rwasa
anatarajiwa kukutana na wafuasi wake katika kile upande wake unasema ni
kuwapatanisha kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015, kwa sababu ananuia kuwania
urais dhidi ya rais Pierre Nkurunzinza.
Rwasa,
ambaye alikuwa mapinzani mkuu wa rais Pierre Nkurunziza wakati wa uchaguzi wa
mwaka 2010 , alisema alihofia maisha yake na hivyo kurejea msituni mwezi Juni
mwaka huo.
Hata
hivyo hali yake haikujulikana tangu hapo, huku baadhi ya ripoti zikisema kuwa
alionekana mpakani katika mkoa wa Kivu Kusini katika Jamuhuri ya kidemokrasia
ya Congo, nchini Tanzania na Zambia.
Upande
wa Rwasa ulikanusha kuwa aliwahi kutoroka Burundi.
Burundi
nchi ambayo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ingali inakumbwa na
athari za vita hivyo vilivyosababisha vifo vya watu laki tatu kati ya mwaka1993
na 2006.
Serikali
imelaumu chama cha FNL kwa mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia huku kukiwa
na madai kuwa Rwasa alikuwa anaanzisha tena uasi dhidi ya serikali.
Chanzo: bbc swahili.

No comments:
Post a Comment