| Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Jimbo Alphonce Mlagara akitoa mwongozo wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Jimbo iliyopo Kichangani. |
| Wajumbe mbalimbali kutoka maparokiani ambao ni viongozi wa halmashauri Walei Parokia wakiwa katika mkutanao huo. |
| Wajumbe mbalimbali kutoka maparokiani ambao ni viongozi wa halmashauri Walei Parokia wakiwa katika mkutanao huo. |
| Aliyesimama ni Katibu wa Halmashauri Walei Jimbo Pascal Bella akisoma muhtasari wa mkutano uliopita. |
VIONGOZI waamini Wakatoliki wametakiwa kuacha kujihusisha na
siasa chafu na badala yake watumie nafasi zao kwa kuwatumikia wananchi waliopa
nafai hizo kwa ajili ya ustawi na huduma mbalimbali za kijamii.
Hayo yamesemwa na Padre Aloyce Mdemu leo katika mkutano wa
tathimini wa jimbo uliosishwa viongozi wa halmashauri ya Walei parokia zote
Jimbo la Iringa uliofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Jimbo Kichangani.
Amesema uongozi wa kijanja hauwezi kuwa na maana kwa
maendeleo ya nchi na badala yake utakuwa ni uongozi wa migogoro isiyo koma.
Amesema baadhi ya viongozi wamekuwa na matumizi mabaya ya
madaraka au mamlaka na kuwafanya wengine kama hawana haki.
Padre Mdemu ambaye pia ni Makamu wa askofu Jimbo la Iringa
na Pasroko wa Parokia ya isimani amesema inafika mahali wengine wanajisahau na
kutumia mabavu katika uongozi na kuifanya migongano katika jamii .
“Madaraka wakati mwingine hulevya sana hasa kwa kujisahau
majukumu yanayopasika kufanywa katika nafasi yako. Kumbe uongozi ni kuwatumikia
watu wote wadogo kwa wakubwa kwa huduma sawa” alisema.
Amesema wajibu wa uongozi ni kutekeleza majukumu yote ambayo
watu wake wanataka kufanyiwa pamoja na kujitoa kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Amewaasa viongozi hao kuwa mafundisho ya Kanisa ni kufanya
mambo yote kwa haki katika nafasi zote za uongozi ndani ya Kanisa na uongozi
ndani ya serikali na kuwataka viongozi kuwa waadilifu.
Amesema uadilifu uanze katika familia ili watoto wakuwe
wakiwa na malezi bora na roho ya utumisho bora kwa wengine.
No comments:
Post a Comment