masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, August 26, 2013

JIHADI INATAFSIRIWA VIBAYA: SHEIKH


Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akijadili na kutoa maelezo juu ya amani katika mkutano uliofanyika jana katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya Iringa.
Baadhi ya watu mbalimbali wakisikiliza mjadala wa amani katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo jana.

Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema Dunia inapita katika ghasia na migogoro ambavyo sababu zake ni uchumi, tofauti za kisiasa na kidini.

Alisema hayo jana katika mkutano wa kujadili amani uliofanyika mkoani  hapa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliojumuisha dini na madhehebu mbalimbali pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali.

Alisema kuwa kumekuwa na kutafsiriwa vibaya na watu mbalimbali wakiwamo waislam wenyewe kwa neno jihadi ambalo wengi wanalitafsiri kama ni kuingia vitani.

“Kwa bahati mbaya inapotajwa jihadi ndani ya vichwa vya waislam wengi na wengi wasio waislamu wanachokidhani wao ni vita tu, kwamba jihadi maana yake ni waislamu kuwa tayari muda wowote na kwa njia yoyote kupambana kwa vita na wasio waislamu” alisema.

Alisema uelewa huu umezua tatizo kubwa miongoni mwa matatizo ya dunia ya leo ambapo baadhi ya makundi ya waislamu hutumia njia zisizo halali kama za wale wanaojilipua mabomu, wakiyalipua mabomu kwa jina la dini katika kuwaua na kuwajeruhi wasio waislamu.

Amekemea vikali vitendo hivyo kuwa ni ukatili usiokubali popote ndani ya waislamu na wote kwa ujumla na kwamba kutokana na mwenendo huu wa hovyo wa baadhi ya waislamu kufanya vitendo hivyo kwa jina la dini, wanaleta taswira potofu na sasa imejengeka ndani ya nchi zisizo za kiislamu na matokeo yake baadhi ya sehemu za jamii zinaongea kwa uwazi.

Alisema vitendo hivi  vimeunda hali ya kutokuwa na imani ndani ya mioyo ya watu na kujenga chuki miongoni mwa watu wasio waislamu kwa waislamu na kwamba kutokana na mwenendo huu wa waislamu wachache, badala ya mambo kuboreka , athari hasi za wasio waislamu zinazidi kuwa mbaya siku hadi siku.

“Kwa vile leo kwa fadhili za mwenyezi Mungu takribani sehemu kubwa ya dunia kuna uhuru wa kuabudu, zikiwemo sheria za umoja wa mataifa na hata hapa nchini petu, basi sababu ya kufikiriwa jihadi kwamba ni vita tu inakuwa haipo.

“Leo jihadi kubwa kwa waislamu ni kujaribu kuyaelewa na kuyatekeleza mafundisho ya dini pamoja na kuyafikisha kwa wengine yaani kufanya mahubiri kwa hekima na mawaidha mema na kujadiliana na wasio waislamu kwa wema” alisema.

Alifafanua kuwa ili dunia iwe na amani ni lazima watu wafanye uadilifu; viongozi wanatakiwa kuwa waadilifu kwa wanaowaongoza na wananchi wenyewe wanatakiwa kuwa waadilifu kwa mamlaka za nchi zao na baina yao wenyewe kwa wenyewe bila kuwekeana fitina, kinyongo au hasira.

Alisema uhuAlisema  matukio haya yanaonu wa kuabudu udumishwe ili watu waweze kuchagua kile wanachokitaka kwa kuwa mara kadhaa kuwanyima watu uhuru wa kuabudu kumekuwa ni kikwazo kikubwa cha kuwepo amani duniani.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema amani itapatikana pale watu watakapo hakikisha hakuna vurugu, hakuna migogoro, hakuna hofu ya vurugu, kukosekana maadui au uadui, endapo hakuna chuki na kutokuwepo ugomvi.

Wakati Mku wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma akifungua mkutano huo alisema kuna matukio yaimu siyo ya kawaida ya uvunjifu wa amani ambayo ni dalili mbaya kuwaenzi waasisi wa amani duniani.

Alisema ili kuwa na amani watu wanapaswa kuwa watulivu kuanzi kwenye familia zao ili kuwaheshimu wengine bila kujali tofauti za kiitikadi za kisiana na kidini.


“Tudumishe amani ili kizazi kijacho kiweze kufurahia amani na upendo na kudumisha amani. Viongozi mbalimbali wa dini na madhehebu hubirini amani” alisema.

No comments:

Post a Comment