masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, August 4, 2013

CHAMA CHA WAPIGA PICHA IRINGA CHAPATA VIONGOZI WAPYA

Waliosimama katikati ni wajumbe walioteuliwa kusimaimia uchaguzi wa viongozi wa chama cha wapiga picha Mkoa wa Iringa.

Thobias Kikulacho akiwashukuru wajumbe wa Chama cha wapiga Picha Iringa.

Uongazi mpya uliochaguliwa kuongoza chama cha wapiga picha Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha miaka mitatu (2013-2016).

CHAMA cha wapiga picha Mkoa wa Iringa kimepata viongozi wapya watakaofanya kazi kwa muda wa miaka mitatu (2013/2016).

Uchaguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Manispaa Said Ng’amilo  (mwenyekiti), Juma Kivambe (makamu mwenyekiti, Thobias Kikula (Katibu), Juma Kivambe (Katibu Msaidizi) na Piusi Agustino (Mhazini).

Wajumbe walimewataka viongozi waliochaguliwa kuwa makini na kutotetereka wala kubabishwa na kitu na kuhakikisha chama kinasonga mbele kwa maendeleo ya baadaye.

Hata hivyo akiongea mara baada ya kuchaguliwa katibu wa chama hicho Thobias Kikula amesema wajumbe wanapaswa kuelewa thamani waliyowapa viongozi wao na kuwa watakitumikia chama kwa misingi ya katiba.

Akiongea baada ya Uongozi mpya Uliwashukuru wajumbe kwakuwa na imaninao na kuwataka wajumbe kuelewa dhamani walioitoa kwao itaheshimiwa kwa kukitumikia chama kwa uaminifu na kujitolea mudawote kwa faida yetu.


Chama cha wapiga picha Mkoa wa Iringa kilianzishwa mwaka 2002 na kusajiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Septemba 12, 2007 kwa namba BST, 3316.

No comments:

Post a Comment