masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, August 1, 2013

GLOBAL OUTREACH TANZANIA YAWAKOMBOA WANAFUNZI IRINGA

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa wakitumia teknolojia ya mtandao kusoma katika maktaba ya Global Outreach.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari wakisoma katika maktaba ya kidijitali.

Jimbo Katoliki la Iringa limedhamiria kuwajibika katika kuboresha elimu kwa njia ya mtandao wa kidigitali katika shule mbalimbali pamoja na watu binafsi wenye nia ya kujiendeleza.

Kupitia maktaba ya kidijitali ya Global Outreach iliyopo Kichangani, wenye ulemavu wa kuona na kusikia watanufaika kwa kuwa na teknolojia ambayo itawawezesha kupata kile wanachokitaka kupitia teknolojia hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Mkurugenzi wa Global Outreach Tanzania Sixtus Kanyama anasema licha ya changamoto mbalimbali wanazozipata, mwitikio wa waalimu na wanafunzi unaridhisha kwa kuitumia maktaba hiyo.

Anafafanua kuwa matumizi ya maktaba ya kidigitali inarahisisha kupata masomo kwa muda mwafaka bila kusubiri vitabu vilivyochapwa kwa kuwa kitabu ambacho kingepatikana darasani na kutumiwa na wanafunzi watatu au wanne kinapatikana kwenye mtandao na kutumika na mwanafunzi mmoja kwa muda mwafaka ikiwa ni pamoja na vitabu vipya ambavyo vinakuwa havijamfikia mwanafunzi na mwalimu.

“Nianze kwa kuwapongeza wanafunzi na walimu ambao wametambua umuhimu wa maktaba hii. Muamko wao ni mkubwa kwa pande zote mbili kwa maana ya waalimu na wanafunzi. Muamko wa wanafunzi hadi sasa unafikia asilimia 50 (50%) wakati walimu ni asilimia 25 (25%)” anasema Kanyama.

Licha ya muamko huo anasema wapo baadhi ya walimu na wanafunzi ambao wanaamini kutumia machapisho pekeke (had materials) ndiyo njia sahihi zaidi.

Anakwenda mbali zaidi na kusema kuwa, pamoja na vitendea kazi kuwepo bado watu wengi hawajaichangamkia teknolojia mpya ambayo jibu la maswali magumu yanayoikabili sekta ya elimu.

“Inaonesha kuwa wanafunzi wengi na waalimu wangekuwa na muamko mkubwa zaidi wa kuitumia teknolojia hii mpya, sekta ya elimu inaweza kukua kwa kiwango kikubwa kwa sababu teknolojia yetu inajibu na kutatua matatizo manne likiwemo la uhaba wa vitabu, uhaba wa walimu, mbinu mbovu za ufundishaji na wanafunzi kubaki kama wapokeaji  tu wa kile kinachofundishwa darasani kwani sasa wanapata nafasi ya kujitegemea” anasema.

Mradi huo ambao uko chini ya Kanisa Katoliki jimbo la Iringa unadhamiria kusambaa kote nchini kutokana na mwitikio na mapokeo ya wengi wanaoonekana kuwa na uhitaji wa kutumia teknolojia hiyo kielimu.

Kanyama anamueleza askofu wa jimbo la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kuwa ni wa aina yake katika kupigania elimu kwa kujitoa kwa kila namna.

“Baba askofu Ngalalekumtwa ni mtu wa aina yake. Hili halina mpinzani kwa wale wanaomfahamu. Ni mtu anayependa elimu na anatumia muda wake mwingi kwa ajili ya kuhakikisha elimu inasonga mbele hasa katika jimbo hili” anasema.

Anatoa mfano wa shule wanachama wa kutumia maktaba ya kidigitali ya Global outreach katika mitihani kuwa ni Mafinga Seminari iliyopo katika Wilaya ya Mufindi, Shule ya Sekondari ya Bomalang’ombe, Image zilizopo katika Wilaya ya Kilolo, shule ya Wasichana Iringa (Iringa girls) na shule ya sekondari ya Lugalo zilizopo katika Manispaa ya Iringa.

“Kupitia shule hizo, zimekuwa kipimo kwetu kwa kuwa na matokeo mazuri. Kipimo chetu kingine ni kwamba, wanafunzi ambao wamekuwa kama viongozi wa wenzao wapo vyuo vikuu” anasema.

Kanyama anasema hivi sasa kuna utaratibu wa kupanua wigo wa utoaji elimu kwa watu mbalimbali wenye ulemavu ili kuwawezesha kupata kile ambacho wengine wanakipata ambapo kwa sasa wenye ulema wa kuona wananufaika kwa kusikiliza kitu kile kile ambacho wengine wanakisoma.

Anabainisha kuwa baadhi ya wadau wa elimu wameridhika na huduma hiyo na kuamua kutoa msaada kwa ajili ya kuwawezesha wenye ulemavu kupata elimu kwa njia ya mtandao.

“Kuna asasi moja inaitwa “Iringa Living Lab” ambayo iko chini ya shirika la Tanza ICT tunafanya nao kazi kwa kwa ajili ya kuboresha maktaba ya kidigitali kwa matumizi ya wenye ulemavu ambapo kila siku ya ijumaa tunatoa mafunzo kwa wenye ulemavu wa wasiosikia ili waweze kupata ujuzi wa kutafuta kile wanachokihitaji kwenye mtandalo.

“Kwa wasioona tunawatengenezea masomo kwa njia ya sauti ili waweze kusikiliza na kujua nini kinaelezwa” anasema.

Pia anasema kuwa wapo katika mpango wa haraka kuwatengenezea utaratibu wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa kuwawezesha kufanya mitihani ya maarifa (QT) kama wengine wanavyo fanya ili wasijione wanyinge na watu waliosahaulika.

Akieleza changamoto wanazokumbana nazo, Kanyama anasema walimu wa Wakuu wa shule wameelewa umuhimu wa maktaba ya hiyo lakini bado kuna hawajawajibika kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha walimu wao katika shule zao na kwamba asilimia 75 (75%) ya walimu bado wanaamini vitabu.

Pia anasema wapo baadhi wanafunzi ambao wanatumia vibaya teknolojia hii kwa kuwa wengi wanapoingia wanakuwa na lengo la kuangali mambo machafu kwenye mtandao badala ya masomo japo kuwa katika upande wa maktaba ya kidigitali wamefanikiwa kufunga mambo hayo na kumsaidia mwanafunzi kujikita katika masomo tu na si vinginevyo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugalo wakiwa katika maktaba ndogo ilipo shuleni hapo inayosimamiwa na Global Outreach wakijisomea kwa njia ya mtandao.

Mary Lugusi ni miongoni mwa wanafunzi ambao wamenufaika na maktaba hiyo na sasa anasoma katika Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM)licha ya wanafunzi watano walionufaika na maktaba hiyo kuwa vyuo vikuu hapa nchini.

Anazungumza na mwandishi kuwa ukaribu wake na Global Outreach ndio ulimuwezesha kupata nafasi ya kujiunga na chuo hicho kwa kuwa alikuwa akipenda sana kusoma kwa kutumia kompyuta.

“Mwaka 2010 nilijiunga na maktaba ya Global Outreach na kutumia maktaba ya kidigitali kusoma masomo mbalimbali. Nilipata upeo mkubwa kwa kuwa kila nilichokuwa ninakitafuta nilikuwa nakipata pamoja na rejea zake ambapo nilipata hamu kubwa ya kufungua kujisomea.

“Maktaba ya kidigitali ina vitabu ambavyo ni msaada mkubwa. Kuna mfumo mzuri wa vitabu vya hesabu na lugha nah ii makta inasaidia kwa wale wanaopenda kufanya mambo yasiyo na maana wasifanye kwa sababu ni ya kisasa zaidi ni maalum kwa taaluma tu ” anasema Lugusi.

Anasema upekee wa maktaba hiyo unaonekana pale wanapokuwa wanajihusisha na wanafunzi kwa kiwango kikubwa bila malipo na kwamba maisha yake kwa sasa ni teknohama.

“Kila kitu kikitumika ipasavyo kina faida lakini sisi watu huwa tunatumia kwa ulimbukeni na kusababisha kitu ambacho kinakuwa msaada kugeuka kuwa ni kitu cha anasa. Haya ni matumizi mabaya ya akili zetu na fikra zetu” anasema.

Anasema kuna haja ya watu wanaotoa huduma za mtandao kuhakikisha wanakuwa na usimamizi kwa watu wanaopata huduma ili kuhakikisha wanafanya kile ambacho kinajenga maadili na akili ya mtu badala ya watu kutumia kwa upuuzi na mambo ya aibu.

Anafafanua kuwa ni jambo la aibu na la kufedhehesha kuona hata wasomi wa vyuo vikuu ambao wanatakiwa kuwa kioo kwa watu wengine wanatumia mitandao vibaya badala ya kutumia katika elimu na maendeleo.

Anasema taasisi na mashirika mbalimbali yanayotoa huduma za kimtandao wawe na mipaka katika utoaji huduma kwa jamii ili kulinda maadili.


“Kutokana na Global Outreach nilianza kujifunza mawasiliano na teknolojia (IT) ndiyo maana nilifanikiwa lakini usije ukafikiri kuangalia picha chafu na takataka zingine unaweza ukapata akili. Hata siku moja! Huo utakuwa ujinga wa kudumu” anasema.

No comments:

Post a Comment