masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, August 12, 2013

BREAKING NEWS!!! COASTER YA KAMPUNI YA ANOTHER G LAUA IHEMI


GARI ya abiria aina ya Coaster kampuni ya another G limegonga mtembea kwa miguu muda mfupi uliopita katika maeneo ya Ihemi Wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa na kupoteza maisha papo hapo.

Gari hilo lenye namba za usajili T 872 BHV lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Njombe limemgonga  John Mhelela mkazi wa kijiji cha Ihemi ambapo inaelezwa kuwa marehemu alikuwa akitoka kilabuni na mara baada ya kuingia barabarani akakutwa na mauti.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa ajali hiyo imetokana na mwendo kasi wa gari.

Daima Mlyuka ameongea na mtandao huu kuwa aliona gari iko katika mwendo kasi japo kuwa mbele kulikuwa na mtembea kwa miguu dereva hakuweza jambo lililosababisha ajali hiyo.

Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa anatoka katika kilabu maarufu kwa jina la “Denyeka” kilichopo kijijini hapo.

“Marehemu alikuwa anatoka kilabu cha Denyeka lakini alipoingia barabarani tukaona gari linakuja kwa mwendo mkali, alipojaribu kulikimbia kwa bahati mbaya likamuwahi kabla hajamaliza barabara likamgonga. Mwendo wa gari ulikuwa wa hatari kweli maana hata sisi tuliokuwa tukiangalia hata kama isingetokea ajli ule mwendo ni mkali mno” amesema.


Ajali imetokea majira ya saa 12:30 jioni na hadi muda huu taarifa zinapelekwa mtandaoni askari wa usalama barabarani hawajafika katika eneo la tukio huku maiti akiwa amenasa chini ya gari.

No comments:

Post a Comment