masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, August 11, 2013

PIGO LINGINE JIMBO LA IRINGA


Padre Liberatus Mwenda wakati wa uhai wake akiongoza wafanyakazi parokiani Nyakipmbo.


Jimbo la Iringa limepata pigo kwa kuondokewa na Padre Liberatus Mwenda Paroko wa Parokia ya Nyakipambo.

Padre Mwenda aliaga dunia Agosti 9 Mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kupata mshtuko (stroke) na kuanguka ghafla alipokuwa parokiani kwake.

Kutokana na mshtuko huo Pd. Mwenda alifanyiwa upasuaji wa kichwa ili kunusuru maisha yake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba.

Katika taarifa zilizotolewa leo Kihesa, mwili wa marehemu unatarajia kuwasili katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Tosamaganga ambako utazikwa Agosti 13 Mwaka huu.

Hivi karibuni jimbo la Iringa lilimpoteza Padre Alphonce Mhamilawa Paroko wa Parokia ya Ifunda.

No comments:

Post a Comment