![]() |
| Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema |
TAARIFA zinazotufikia sasa ni kwamba cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi katika kata nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kalolei Arusha.
Uchaguzi ho umefanyika leo katika
kata hizo baada ya kuahirishwa Juni 16, Mwaka huu baada ya kutokea kwa mlipuko
wa bomu katika mkutano wa Chadema kuhitimisha kampeni.
Katika uchaguzi huo kulikuwa na
ushindani mkali katika ya Chadema na chama cha Mapinduzi (CCM).
Wachambuzi wa siasa wanasema
kutokana na ushindi wa Chadema unaweza kusaidia chama hicho kushinda katika
kiti cha Umeya katika jiji hilo.
Jumla ya vyama vya siasa 5 vimeshiriki uchaguzi huo.

No comments:
Post a Comment