masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, July 16, 2013

SIMANZI NA VILIO UASKOFUNI IRINGA

Jeneza likiwa nje ya nyumba ya marehemu kijijini Ihimbo baada ya kushushwa kwenye gari kabla ya ibada ya kuanza kwa ajili ya kuelekea makaburini. 

Padre Aidan Ulungi akiongoza ibada ya mazishi nyumbani kwa marehemu kijijini Ihimbo kabla ya kuelekea makaburini kuzika.

Jeneza likishushwa kaburini ili kazi ya kuzika ianze.

Jeneza likiwa limeshashushwa kwenye kaburi tayari kwa kuzika.

Mke wa marehemu akiweka shada juu ya kaburi,

Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua juu ya kaburi.

Christian Sambagi na Faustino Kitosi wakiweka shada juu ya kaburi kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.

Masista wakiweka shada juu ya kaburi.

Padre Aidan Ulungi akiwa na mwenzake Pritas Chelula wakiweka chada juu ya kaburi.
WAFANYAKAZI wa uaskofuni Jimbo Katoliki la Iringa wapata simanzi kubwa kutokana na kufiwa kwa mfanyakazi mwenzao Izack Mgaya.

Mgaya ambaye alikuwa ni fundi wa magari alifariki Julai 14 asubuhi na kuzikwa Julai 15 mwaka huu kijijini kwake Ihimbo.

Akiongea makaburini wakati wa mazishi Padre Aidan Ulungi ambeye ndiye mwajiri alisema Mgaya ameacha pengo kubwa ambalo halitazibika kutokana na uchapakazi wake.

Ulungi alisema kazi nyingi zilizokuwa zikifanywa na Mgaya zimesimama kwa kuwa hakuna wa kuziba nafasi hiyo na kwamba hata akipatikana hatofikia kiwango alichokuwa nachoa.

“Kwa muda wote ambao nimemfahamu Izack na niliofanya naye kazi, lazima nikiri kuwa nafasi yake si rahisi kuiziba kutokana na uchapakazi wake na uwajibikaji wa dhati.

Izack alikuwa ni mwaminifu kwa kazi ambazo alizokuwa akipewa, alijituma kwa dhati. Pia hakuwa ni mtu wa kulalamika bali alitumia muda wake kwa uadilifu mkubwa. Hizi ndizo sifa zake na hata Mungu atampokea kwa hilo” alisema Ulungi.


Mara baada ya mazishi kumalizika Pd. Ulungi aliahidi kusomesha watoto wa marehemu watatu.

Mgaya alikuwa mkuu wa kitengo cha ufundi magari na May Mosi mwaka huu alipata zawadi na cheti cha ufanya kazi bora.

Hata hivyo ameacha watoto 5, wakike wawili na wakiume 3 pamoja na mjane mmoja.

Mgaya alifariki baada ya kusumbuliwa kwa takribani miezi mitatu akisumbuliwa na upungufu wa damu mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment