masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, June 3, 2013

WANAWAKE 454 HUFARIKI DUNIA WAKATI WA KUJIFUNGUA KILA MWAKA


JUMLA ya wanawake wajawazito 454 hufariki dunia kati wanawake 100,000 wanaojifungua nchini kila mwaka.

Haya yamezungumzwa na mkufunzi wa idara ya afya taifa Januari Soko alipokuwa akiongea na wadau wa sekta ya afya katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa leo.

Soko alisema katika sekta ya afya kunachangamoto za utoaji huduma kwa ushirikiano na taasisi binafsi pamoja na mashirika ya dini jambo ambalo linazidi kuwatesa wananchi.

Ametaja sababu zinazokwamisha kuwa ni uelewa juu ya haki hakisi ya huduma, wadau mbalimbali kuwa na mtazamo hasi juu ya huduma zinazotolewa, kutokuwa na vipaumbele katika utoaji huduma na kukosa sera na mpango wa utoaji huduma.

Amewataka wadau mbalimbali wa afya kutoa huduma bila kuwa na mgongano ili kuweza kupanua huduma kwa wananchi kuwahudumia wananchi bila manung’uniko.

Ahata hivyo amesema kuwa nusu ya akina mama hujifungulia hospitalini huku vifo vya watoto wenye umri wa mwaka mmoja ni 51 kwa kila watoto 1000.

Wakati akieleza hayo, taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa imeeleza kuwa kwa mwaka 2012 vifo vya akina mama wajawazito ni 223 kati ya 100,000 wanaojifungua kimkoa huku vifo vya watoto wenye umri wa mwaka mmoja ni 18 kati ya watoto 1000.

Taarifa hizo zinaonesha kuwa magonjwa kwa watoto ni asilimia ishirini (20.6%) ambapo watoto wengi wanaouguwa na kulazwa husumbuliwa na ugonjwa wa maralia.

Katika utoaji huduma za HIV, taarifa hiyo imeeleza kuwa katika mkoa wa Iringa umefikisha asilimia tisa (9.1%).

Wakati akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Iringa Leticia Warioba amesema takwimu za utoaji huduma za afya kitaifa za mwaka 2012 zinaonesha kuwa sekta binafsi inamiliki vituo 1738 sawa na asilimia 27.4 ya vituo vya huduma za afya katika nchi yetu.

Hata hivyo amesema zimo hospitali 137 kati ya hospitali 240 sawa na asilimia 57.1, vituo vya afya 189 kati ya 633 sawa na asilimia 29.9 na zahanati 1,412 kati ya 5,469 sawa na asilimia 25.8.

Katika takwimu za Mkoa wa Iringa za mwaka 2012 zinaonesha kuwa kuna hospitali 4 za sekta binafsi kati ya hospitali 7 sawa na asilimia 57, vituo vya afya 8 kati 21 sawa na asilimia 38 na zahanati 56 kati ya 226 sawa na asilimia 4.8.

Utoaji wa huduma kitaifa hadi sasa, serikali inatoa kwa asilimia 69.6 (69.6%), mashirika ya dini yanatoa kwa asilimia 13.6 (13.6%0 na sekta binafsi wakitoa kwa asilimia 13.8 (13.8%).

No comments:

Post a Comment