HALI ya mazingira katika Mkoa wa Iringa hairidhishi kutokana na watu kutowajibika kikamilifu katika utunzaji mazingira pamoja na kujenga vyoo bora.
Haya yamezungumzwa leo na Mkanga Mkuu wa Mkoa Salim Robert alipokuwa akifungua kikao cha wadau cha kujadili kampeni ya usafi wa mazingira kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha afya mkoani hapa.
Robert amesema katika halmashari bado hakujawa na hali ya kuridhisha na jambo linaloweza kusababisha madhara ya mlipuko wa magonjwa kwa wananchi hususani kwa wanafunzi wa shule mbalimbali ambao wanakubwa na adha kubwa ya uhaba wa vyoo.
“Hali ya mazingira ni changamoto kubwa kutokana na ongezeko la watu. Hii ni pamoja na vyoo vyetu kutokuwa bora na upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo kwa wananfunzi mashuleni na kusababisha wananfunzi ujisaidia hovyo na usafi kwa ujumla” amesema.
Amesema wananchi bado wana uelewa mdogo juu ya kutunza mazingira hali inayosababisha kutupa taka hovyo.
Kwa upande wake Ofisa afya wa Mkoa wa Iringa Khadija Haroni amesema hali ya usafi kwa upande wa mji inazidi kuimarika japo kuwa kwa upande wa vijijini bado hakujawa na mabadiliko.
Amesema licha ya takwimu kuonesha kuwa juu kwa ufanisi wa kuwa na vyoo, kati ya vyoo hivyo vilivyo bora ni asilimia kuni na 12 (12%) tu ambavyo ni bora.
“Tunapozungumzia vyoo, hatumaanishi ili mradi vyoo tu, bali tunalenga vyoo vilivyo bora. Vyoo bora ni vile visivyo ruhusu muingiliano wa kinyesi na binadamu” amesema.
Amesema kuwa licha ya elimu kuendelea kutolewa, watu wanatofautgiana kimtazamo na upokeaji wa welimu hiyo jambo ambalo linarudisha sana maendeleo.
Amesema Mkoa umeandaa mbinu maalumu ambayo itakuwa shirikishi kwa wananchi itakayomuwezesha mtu binafsi kubadilika.
“Mpango huu tunategemea utasaidia sana uhamasishaji wa mtu biafsi na kushiriki kikamilifu katika utunzaji mazingira pamoja na wale wanaojenga nyumba waweze kujenga vyoo vinavyosafishika” amesema.
Kwa upande wa mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa aliyehudhuria kikao hicho Donard Mshani amesema kwa upande wa vijijini shule zinakabiliwa na changamoto kubwa za kimazingira ambazo zinasababisha wanafunzi kutozingatia masomo wakati wa vipindi.
“Kuna tatizo kubwa la vyoo ambapo hata hivyo ni shule chache tu ambazo zina maji. Suala la mazingira ni muhimu katika maendeleo ya taifa kwa sababu watu wanapokuwa wananumwa hakuna shughuli ambazo zinaweza kufanyika kwa ajili ya maendeleo” amesema Mshani.
Shirika la UNICEF kwa kushirikiana na Mkoa wa Iringa wameanda kampeni ya uhamasishaji wa utunzaji mazingira kwa wadau mbalimbali pamoja na wananchi ambapo kikao hicho ni cha siku mbili kilichoanza leo na kinatarajiwa kufungwa kesho.

No comments:
Post a Comment