masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, June 1, 2013

WAFUASI WA CCM WAVAMIA NA KUJERUHI NG'ANG'ANGE

Rais Jakaya Kikwete



WATU watatu ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamepigwa na kujeruhiwa na watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kijiji cha Mdeke Kata ta Ng’ang’ange jimbo la Kilolo.

Kipigo hicho kimetokea leo mita 50 kutoka ofisi ya Chadema ambapo wanchma wa Chadema walikuwa wamekaa kufanya maongezi yao nyuma ya ofisi.

Wakati vurugu hizo zikianza mwanachama mmoja wa Chadema alikuwa akipita barabarani jirani na uwanja walipokuwa wakifanyia mkutano CCM ambao hutumiwa na Chadema kufanyia mkutano.

Wakati mwanachama huyo akipita alijikuta akivamiwa na kundi la vijana wa CCM na kuanza kukimbia kuelekea ofisini kwao ambako wenzake walikuwa wakifanya maongezi  hali iliyosababisha wengine kupigwa bila kutegemea.

Wakati tukio hilo likitukia viongozi wa CCM walitumia mgambo kwenda kuwadhibiti wanachama wa Chadema kwa hofu kuwa wangerudisha mashambulizi jambo ambalo mgambo walijikuta wakiwa na hofu kuwakamata bila sababu na kulazimika kupiga simu kituo cha Polisi Kilolo kwenda kutoa msaada.

Watu waliopigwa ni Fahamu Mgata ambaye alikutwa na dhahama hiyo wakati akijiandaa kutoka na pikipiki ya matangazo kwenda kutangaza mkutano wa Chadema huku ambapo aliyekuwa akipita jirani na mkutano huo kwenda kujumuika na wenzake katika maongezi ofisini na kuanza kupata kichapo ni Tomasi Msuva.

Chagua Lwisa ni majeruhi wa tatu ambaye pia alikuwa ameumizwa wakati akijaribu kumuokoa Msuva aliyekuwa akiwakaribia huku akipokea kichapo.

Kada mmoja wa CCM aliyehojiwa na mtandao huu na kuomba jina lake lisiandikwe amesema kuwa mpango huo umepangwa kwa kufanyika hivyo kila wakati kwa lengo la kuwakatisha tamaa wananchi kukipigia kura Chadema.

“Kwanza naomba unilinde, mimi nipo ndani ya CCM lakini kwa mipango ya kampeni inayopangwa sasa si mizuri kwa sababu ni kutumia fujo. Watu wa leo hawahitaji siasa za fujo bali wanataka siasa za hoja lakini tulipofikia ninalaani kabisa kitendo hiki.

“Mlengwa mkuu katika hili ni Baraka Mfilinge na Tomasi Msuva wa Chadema kwa kuwa ndio wanaosadikiwa kuwa wanafanya siasa za kuwabadilisha wananchi kuhamia Chadema. Kiukweli huu siyo uungwana. Ifike mahali tukishindwa tukubali kuwa tumeshindwa kuliko kutumia mabavu” kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo mtandao huu ulifanikiwa kuongea na baadhi ya maaskari wa Kilolo ambao majina yao tunayo (yanahifadhiwa) wallisema walipigiwa simu kwa ajili ya kwenda kuwakamata wafuasi na wanachama wa Chadema jambo ambalo walipofika wakaona ni la uonezi.

Hata hivyo chanzo hicho kimeeleza kuwa hayo yanatokea baada ya kuona mbinu za kumrubuni mgombea wa Chadema zinagonga mwamba baada ya kushtikiwa.

“Mtu mmoja mkubwa tu wa CCM alitupigia simu kuwa tukifika kule tumkamate Baraka Mfilinge, Tomasi Msuva na mwandishi wao lakini kiukweli baada ya kufika pale tuligundua kuwa CCM ndio wachokozi.

“Uchokozi wa CCM unakuja pale walipokwenda kufanyia mkutano nje ya ofisi ya Chadema lakini hata hivyo wamefanya makosa kuwapiga wanachama wa Chadema kwa kuwa walikuwa katika maeneo yao sahihi” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kilipoombwa kutaja jina la mwandishi wa habari ambaye alitakiwa kukamatwa, kilisema “mwandishi wa gazeti la Tanzan Daima" bila kutaja jina lake.

Vurugu hizo zinatokea siku chache baada ya kuwa na taarifa kutoka ndani ya CCM kuwa kuna watu maalumu kutoka  ndani ya chama hicho wameandaliwa kuhakikisha mgombea wa Chadema Nafred Lucas Chahe anarubuniwa kwa njia yoyote na kwa gharama yoyote ili mradi tu asishiriki uchaguzi kwa kuwa ndiye anayependwa na wananchi.

Hata hivyo mtandao huu umebaini watu ambao wanafanya mipango ya kumrubuni mgombea huyo ambao namba za simu zao zinahifadhiwa na majina yao.

Hata hivyo wananchi walioshuhudia tukio hilo wamelaani vikali na kulazimika kuondoka katika viwanja hivyo huku wakisemezana kuwa CCM imekosa mvuto.


“Kila wakati wanasema Chadema ndio wenye fujo kumbe tulikuwa hatuelewi. Leo tumejionea kwa macho yetu CCM wakianza kumpiga mtu bila sababu. Mbona watu wa Chadema tunao hapa kila siku hatuoni wakianza kumpiga mtu lakini kwa macho yetu tumewaona CCM wakiwapiga. Kama hawakutaka apite hapa barabarani walitaka akapite wapi? Kumbe tumegungua njama zao” zilisikika sauti za   wananchi hao wakisemezana.

No comments:

Post a Comment