masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, June 25, 2013

UNYAMA HUU UNAVUMILIKA?





HAKI za binadamu zinazoliliwa kila siku katika vyombo vya haki na vya sheria ziko wapi hasa katika nchi ya Tanzania?

Vyombo vya usalama kazi yake nini ikiwa watu watu wanapodai haki zao wanafanyiwa unyama kama huu? 

Maswali kama haya kuenda wapo wengine ambao wakawa nayo kichwani lakini wakawa wanaogopa kuuliza au wapo wale ambao wanaweza kutoa majibu yake.

Unyama huu wanafanyiwa watu wa Mtwara ambao hivi karibuni walikumbwa na dhahama ya kipigo wanaoomba kujua hatima ya ujenzi wa kiwanda cha gesi unaoleta mkanganyiko wa wapi kitajengwa.

Hivi ni nami mhalifu kati ya yule anayedai haki na yule anayeliibia taifa?

Wapo watu wanaotuhumiwa kwa upotevu wa mamilioni ya pesa za umma kupitia Benki Kuu (BoT), EPA, Kagoda na sehemu kadha wa kadha lakini hajaonekana hata mmoja anayeteswa kama hivyo wanavyoteswa wananchi wa Mtwara.

Je, haki iko zaidi kwa watu gani wa kada gani na wa nyadhifa gani?

Huenda wapo waungwana wanaoweza kutoa majibu ya maswali hayo.

No comments:

Post a Comment