WANAFUNZI wa chuo kikuu cha
Tumaini Mkoani Iringa wameshiriki katika kusaidia ukuaji wa elimu
vijijini kwa kutumia nguvu zao katika ujenzi wa maktaba inayojengwa katika
Wilaya ya Kilolo.
Wanachuo hao wametoa ushirikino
wao kwa asasi isiyo ya kiserikiali ya Tuwafikie Tanzania inayojihusisha na
uhamasishaji wa elimu vijini.
Akizungumza na mtandao huu,
mhamasishaji wa asasi hiyo Bovan Mwakyambiki amesema jamii itambue kuwa kukua
kwa elimu kunahitaji watu wanaojitoa.
Amesema ushiriki wa wanafunzi
wa chuo Kikuu cha Tumaini uwe ni mfano kwa jamii na kutumia muda wao katika
kukuza vipaji hasa katika elimu.
Amese jamii yetu itakuwa na
uwezo wa kujitegemea endapo itakuwa na
akili ya kung’amua mambo na upambanuzi wa mambo mbalimbali katika maisha ya
kila siku.
Maktaba hiyo inajengwa katika
maeneo ya Lugalo Wilaya ya Kilolo ambapo itakuwa ikitoa huduma kwa kila mtu
hasa elimu ya jamii kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment