masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, June 18, 2013

MAPAMBANO MAKALI ARUSHA,LEMA ANUSURIKA KUUAWA,

HALI tete katika jijini la Arusha muda huu,Polisi wanapiga mabomu ovyo,watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Soweto wakisubiri kuaga miili ya watu waliofariki dunia katika shambulio la kigaidi wametawanywa kwa mabomu.

Mbali na watu kutawanywa kwa mabomu hayo,Mbunge wa Arusha Mjini Godless Lema amenusurika kufa huku gari lake likiharibiwa vibaya na mabomu ya Polisi .
Mwandishi wa Blog hii  akiwa eneo la tukio ameshuhudia majeruhi kibao wakikimbizwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.
Barabara kuu ya kuingia mjini imefungwa, mabomu yanapigwa kila kona jijini Arusha risasi za moto zinatumika.

Akizungumza na Blog hii katika eneo la tukio mmoja wa wahanga wa tukio hilo, Agnes Mosha anasema kwamba hajui walipo ndugu zake wawili waliokuwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuaga miili ya rafiki zao.

"Dada nisaidie nivuke barabara nikimbie Mount Meru nasikia kuna dada yangu amepigwa bomu na hali yake ni mbaya sana,siwezi kuvuka dada sina nguvu tena jamani"alilalamika Agnes mbele ya Mwandishi wa Blog hii  kisha akapoteza fahamu na kuanguka chini.

Hata hivyo baada ya Agnes kuanguka chini hakuweza kuinuka huku watu wakikimbia na kumkanyaga,kulingana na hali kuwa mbaya eneo hilo mwandishi wa Blog hii  pia alilazimika kukimbia nakutafuta eneo la kujificha.

Pia kuna tetesi kuwa katika mapambano hayo kati ya raia na askari polisi, inasemekana askari wawili wameuwawa ingawa taarifa za kuuawa kwa askari hao hazijathibitishwa. Kwa taarifa zaidi endelea kutufuatilia.

No comments:

Post a Comment