Siku
moja baada ya kumalizika uchaguzi katika kata ya Ng’ang’ange, siri ya ushindi
wa chama cha mapinduzi imefichuka. Makada wa chama hicho na wananchi wamefichua
siri hiyo kuwa mchezo mchafu uliochezwa ndio uliowapa ushindi huo.
Wakisimuliana kilabuni katika kilabu cha pombe cha kwa Mitumba kilichopo katika
kijiji cha Mdeke katika kata hiyo ya Ng’ang’ange, wananchi walisema walipewa
fedha shilingi 5,000 kwa kila mmoja ili wampigie mgombea wa CCM.
Licha
ya kupewa pesa hizo usiku wa kuamkia jumapili ya juni 16, wameeleza pia kuwa
wakati wakienda kupiga kura, mabalozi na wenyeviti wa vitongoji walikuwa
wanawagawia shilingi 2,000 kila mpiga kura. Akisimulia watu kwa magambo, mke wa
aliyekuwa diwani wa kata hiyo kabla ya kifo Felechina Msolla amesema watu wa
Ng’ang’ange ni wa pombe tu. “kampeni za hapa Ng’ang’ange ni pombe tu wanaridhika”
alisema Msolla.
Msolla alisema licha ya watu kuridhika kwa pombe,
Chadema kimesababisha hasara kubwa kwa CCM kutokana na kashikashi zake.
"Ila tuseme ukweli Chadema wametupeleka mbio, na tungezembea kidogo tu
kutumia mbinu ya kugawa pesa ingekula kwetu” alisema.
Uchaguzi wa diwani uliofanyika katika kat hiyo
Namgelesi Msuva (CCM) alishinda kwakura 686 dhidi ya Nafred Chahe (CHADEMA)
aliyepata kura 217.
No comments:
Post a Comment