Chama cha
Mapinduzi (CCM) kata ya Ng’ang’ange wameingia katika mgogoro wa wao kwa wao
baada ya kuwahujumu mawakala wao. Hujuma hiyo imetokana na chama hicho kutumia
majina ya watu wengine kwa mawakala waliopewa nafasi za uwakala uwakala.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Batista Mnyalape alisema jina lake
limehujumiwa japo kuwa tume ya uchaguzi ililipitisha. ”Walitangaza nafasi hizo
nikaomba na jina likapitishwa lakini baada ya majina kurudishwa kamati ya siasa
ya kata wamelificha na kumpa mtu mwingine. Kweli nimeamini kuwa CCM ni chama
cha wababaishaji na wahujumu” alisema. Alisema ingawa yeye ni mwana CCM,
ameamini kuwa chama hicho ni chama cha wababaishaji na wahujumu. Kwa mujibu wa
majina ya mawakala waliopitishwa na tume ya uchaguzi, jina la Batistani Mnyalape
ni la 7 kati ya majina 28. uchaguzi mdogo wa diwani unatarajiwa kufanyika Juni
16 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment