masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, June 10, 2013

MAMBO YAMEIVA UCHAGUZI WA UDIWANI KATA YA NG'ANG'ANGE

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mji Mwema katika kijiji cha Mdeke kata ya Ng'ang'ange Ambwene Mbogo amesema wenyeviti wa vitongoji wanakuwa wakufanya kazi bila kuthaminiwa. Alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Chama cha Demokrasia(Chadema) kijijini hapo kumnadi mgombea wa udiwani. Alisema tangu aanze kazi mwaka 1998 amekuwa mtumwa licha yakufanya kazi bila kuthaminiwa. "Tangu nianze kazi mwaka 1998 chini ya CCM, nimekuwa mtumwa. Nfanya kazi kwa mateso makubwa sijapata kuona. Kila wakati sisi vitongoji tunaonekana tunawatesa wananchi kumbe sisi tunatumwa tu wala haatufaidiki na kitu chochote" alsema Mbogo. Aliisukumia CCM tuhuma kubwa kuwa haijui kuajiri huku kikitumia vitisho kutoa maagizo ya ukandamizaji kwa wananchi. "Serikali yao ni ya undugu na mambo yao ni ya kindugu tu." Habari ya CCM kwangu kuanzia leo sasa basi" alisema Mbogo... Wakati akisema hayo Castory Mhagama(45) alisema kuna mateso mengi ambayo yanatokana na mfumo mbovu wa uongozi uliopo na kwamba mfumo huo usiporekebishwa utaliangamiza taifa. "Mateso tunayo, kuna wazee, wajane na watoto ambao wanatelekezwa kwa sababu hakuna mtu wa kuwasikiliza na kuwasemea." "Siwezi sirudishi kadi ya CCM ila kura zote tumpe Nafred Chahe atatusaidia mateso tuliyo nayo" alisema akimnadi mgombea udiwani huyo, mwakilishi wa Mbunge wa Ubungo Ally Said Makwilo alisema umasikini walio nao watanzania adui mkubwa ni CCM. "Ukiwa kiongozi wa CCM  Mwenyezi Mungu kuna vitu fulani anapunguza katika kichwa ndio maana viongozi wa chama hicho hawana fikra za uzalendo wa taifa na kuwaza kuiba tu. Tubadilike ili mwenyezi Mungu atubariki na kutuongezea hekima" alisema.... Alisema Nafred atakuwa kama mbwa wa kuwindia kwani atadhibiti ubadhilifu wa mali ya umma unaofanywa na viongozi wezi. "Mpelekeni Nafred iliawe mbwa akawafulumue ngedere kwenye halmashauri ya Kilolo" alisema. Naye ngombea wa udiwani kupitia Chadema Nafred Chahe amewataka mwananchi wamuamini na kumpa ridhaa ili awatumikie kwa unyenyekevu wa dhati. "Katika elimu tusiwalaumu walimu kwa kuwa wao wanatekeleza maagizo tu. Nawaombeni kura zenu ili tubadilishe mfumo dhalimu" alisema. Hata hivyo mke wa mgombea huyo Maria Msuva alimuombea mume wake kura alisema mume wake anaweza na yeye atakuwa mshauri wake katika kuitumikia jamii na hivyo wananchi wampe kura ili afanye kazi.

No comments:

Post a Comment