Wednesday, June 12, 2013
WANANCHI WATAKIWA KUCHAGUA KIONGOZI ALIYE BORA
MGOMBEA udiwani katika kata ya Ng'ang'ange kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Nafred Chahe amesema yuko tayari kuchapwa viboko endapo atashindwa kuwatumikia wananchi pindi atakapokuwa diwani. Chahe ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ng'ang'ange alipokuwa akiomba kura. Alisema hatasita au kuona aibu kuadhibiwa kwani itakuwa haki yake kuwajibishwa. "Mkinipa ridhaa ya kuwatumikia nikashindwa niadhibuni bila kuogopa" alisema. Naye Mbunge wa Mbozi David Silinde alisema hakuna hakuna dharau iliyo kubwa duniani kama kununuliwa kwa kuwa hudharirisha nafsi ya mtu. "Sisi wanasiasa kwa muda wa miaka mitano tumekuwa waongo kupindukia. Leo hii tunaendeleza uongohuo huo wa miaka hamsini iliyopita" Alisema Silinde. Amewataka wananchi wanapofanya maamuzi ya kuchagua kiongozi waangalie mstakabali mzima wa maisha yao ili kufanya uchaguzi sahihi....Alisema kiongozi mzuri nin yule mwenye hofu ya Mungu ila yule anayeingia madarakani kwa rushwa ni chaguo la shetani. Kwa upande wake Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa akimnadi mgombea huyo alisema zaidi ya watu milioni 30 wanaishi kwa kiwango cha chini kabisa cha umasikini kwa sababu ya kukosa viongozi waadilifu. "Tunaomba mmuchague ndugu yenu Chahe ili aweze kusimamia maendeleo yenu, Msikubali kurubuniwa kwa shilingi 50 kwa kuwa mkifanya hivyo mtakuwa mnajichimbia kaburi lenu wenyewe" Alisema. Alisema kuendelea kuchagua Chama Cha Mapinduzi ni janga la taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment