masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, May 16, 2013

MCH. MSIGWA: KUWANYANYASA MACHINGA SASA BASI


Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa katika Mkutano wa serikali uliofanyika hivi punde katika maeneo ya stendi Kuu ya mabasi kuwataka wafanyabiashara wadogo (Machinga) wasinyanyaswe.


MBUNGE wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa (CHADEMA) ameendelea na msimamo wake wa kuwataka wafanyabishara ndogondogo Machinga katika maeneo ya Mashine tatu katika Manispaa ya Iringa ili kupunguza ugumu wa maisha unaowakabili katika familia zao.


Mch. Msigwa ameyazungumza hayo leo katika mkutano wa serikali uliofanyika stendi Kuu ya Mabasi uliomalizika hivi punde ili kujadili mwafaka wa wafanyabiashara hao wanaozuiliwa kwa nguvu ya dola ili wasifanye biashara zao.


Licha ya kuwa mkutano huo ulitakiwa kuakutanisha viongozi wa Halmashauri na madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri, Meya pamoja na madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekula kona na kuususia mkutano licha ya kuwa wananchi walikuwa na hamu kubwa ya kutaka wajibu maswali yao.


Amesema hajabadilisha msimamo wake juu ya wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara katika maeneo hayo kwa kuwa maisha yanaendelea kuwa magumu.


“Msimamo wangu haujabadilika wala haujawah kubadilika. Wafanyabiashara endeleeni kufanya biashara kama polisi wanataka kuwakamata waje wanikamate mimi tena wanikamatie hapahapa jukwaani wasije nyumbani kama walivyofanya kwa Lema” amesema.


Akizungumza katika mkutano huo, Mch. Msigwa alisema kiongozi mzuri ni yule anayefanya jitihada za kutatua matatizo na si kutumia nguvu kuwaongoza watu.


“Chama cha Mapinduzi wanafikiri kutatua matatizo ni kutumia polisi kupiga watu tu. Tatizo iliyopo nchini ni ukosefu wa ajira lakini watu wanapojishughulisha, waache waendelee kupata chochote kwa ajili ya familia zao na si kuwapiga” amesema Msigwa.


Amesema ni dhambi kuwatumia wananchi wakati wa uchaguzi na pindi uchaguzi unapokwisha kuwatelekeza bila kuwasaidia pale wanapotoa kilio chao hususni wapohitaji kuwatumia viongozi waliowachagua kwa ajili ya kuwapelekea kero zao mbele a maamuzi.


“Wakati wa uchaguzi watu wanatumika vizuri huku wakiombwa kura kwa kupigiwa kagoti bila kujali mtu an umri gani lakini uchaguzi unapokwisha wananchi hutelekezwa na hata madiwani huwakimbia wananchi. Hii ni dhambi kubwa sana” amesema.


Amemtaka kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kutoendeleza tabia yake ya kuleta matatizo ndani ya Mkoa na kwamba mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi hakijasahaulika.


“Namuagiza Kamuhanda, pamoja na tuhuma nyingi za kumuua Mwangosi tusingependa atuletee matatizo mengine haka hayo. Eti kuna usalma gani wa wataifa wanaomshauri Kamuhanda kuendelea kuua wananchi? Kuwafukuza machinga wasifanye biashara ni kuwauwa wananchi” amesema.


Msigwa amewataka jeshi la Polisi kufanya kazi kwa weledi bila kushinikizwa na wanasiasa kuwanyanyasa wananchi huku akisema atachapa fomu za kusaini wale wote ambao haana imani na Kamuhanda ili apelike hoj binafsi bungeni jmbo lililoibua hisia za watu na kumtaka hata kesho zipitishwe.


“Nitachapa fomu za kutokuwa na imani na Kamuhanda ambapo wananchi nitawaomba mzisaini ili nipeleke hoja binafsi” amesema Msigwa huku wananchi kwa sauti wakijibu “Ndiyooooo!!! Hata kesho”.


No comments:

Post a Comment