![]() |
| Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) akielekea kwenye chumba cha mahakama baada ya kushuka kwenye gari. Wanawake wawili mbele yake ni miongoni mwa washtakiwa. |
![]() |
| Abuu Changawe maarufu kwa jina la Majeki akiingia mahakamani mara baada ya kushuka kwenye gari. |
![]() |
| Mbunge wa Msigwa akiwa amebebwa na wafanyabiashara na wananchi mbalimbali mara baada ya kutoka mahakamani na kuelekea katika ofisi ya chama ya Wilaya. |
![]() |
| Mbunge wa Msigwa akiwa amebebwa na wafanyabiashara na wananchi mbalimbali mara baada ya kutoka mahakamani na kuelekea katika ofisi ya chama ya Wilaya. |
![]() |
| Mch. Msigwa akiwahutubia wananchi nje ya ofisi ya chama baada ya kutoka mahakamani. |
MBUNGE
wa Iring mjini Mch. Peter Msigwa (CHADEMA) na wafanyabiashara 75
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya wakikabiliwa na makosa
matatu .
Msigwa
anakabiliwa na makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni la kwake pekee
yake na huku kosa la pili likiwahusu washtakiwa wote.
Akisoma
mashtka hayo mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya
Godfrey Isaya, mwendesha mashta wa serikali Adolf Maganda alisema Peter
Msigwa ambaye ni mshtakiwa namba moja anakabiliwa na shtaka la
kushawishi watu kutenda uhalifu ambapo alisema Msigwa alifanya ushawishi
huo katika mkutano alioufanya Mei 15 Mwaka huu katika maeneo ya
mashinetatu.
Kosa
la pili ambalo linawakabili watuhumiwa wote 76 limetjwa kuwa watuhumiwa
walifanya mkusanyiko pasipo kibali cha polisi na kusababisha uhalifu
kufanyika ambapo alisema Mei 19 Mwaka huu watuhumiwa walikusanyika
katika maeneo ya mashine tatu bila kibali.
Akisoma
kosa la tatu Maganda alisema linawahusu watuhumiwa namba 2 hadi 76
ambapo alisema mnamo Mei 19 Mwaka huu watuhumiwa waliharibu kwa makusudi
gari lenye namba za usajili SM 9323 mali ya zimamoto.
Baada
ya kusomewa makosa yao, wakili wa kujitegemea ambaye pia ni wakili wa washtakiwa Bazil Mkwata alisema
makosa wanayokabiliwa nayo wateja wake yanadhamana na hivyo kuiomba
mahakama wataja wake wapewe dhamana.
Akitoa
masharti ya dhamana hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Godfrey Isaya
amewataka washtakiwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika
ambaye anatakiwa kuwa na shilingi milioni moja na kwamba washtakiwa hao
wakipewa dhamana wasijihusishe na uhalifu tena.
Hata
hivyo mwendesha mashtaka huyo alisema upelelezi haujakamilaka na
watuhumiwa 49 wapo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana
huku washtakiwa 27 wakirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana na kesi
hiyo itatajwa tena Juni 3 Mwaka huu.
Washtakiwa
hao wamepandishwa kizimbani siku moja baada ya kukamatwa katika
purukushani za askari kuzuia wafanyabiashara ndogondogo (Machinga)
kufanya biashara zao katika maneo ya mashinetatu.
Katika
mkutano wa kiserikali uliofanyika 19 Mei Mwaka huu katika maeneo ya
Mashinetatu Msigwa alisisitiza Machinga kutoondoka katika maeneo hayo
ili waweze kufanya biashara kwa ajili ya kupata chochote kwa ajili ya
familia zao.
Mara
baada ya kutoka mahakamani wafanyabiashara na wananchi walimbeba mbunge
wao hadi ofisi ya chama iliyopo Msindo ambako aliongea na wnanchi.
Akiongea
na umat wa wananchi Msigwa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano
waliouonesha kwake na kwa wafanyabiashara tangu mwanzo wa tukio hadi
mwisho kwa kile alichosema wameonesha uzalendo wa dhati.
“Ninawashukuru
sana wananchi kwa uzalendo wenu japo kuwa kuna watu wangu wamekosa
dhamana lakini nawaahidi kuwa kesho (leo) nitafanya jitihada zozote kwa
kushirikiana na viongozi wenzangu kuwatoa. Ila niwatoe wasiwasi kuwa
waliobaki watatoka” amesema Msigwa.
Kwa
upande wake wafanyabiashara wamemfananisha Msigwa na Mwalimu Nyerere
kwa moyo wake wa dhati na upendo wa kweli kwa kile walichosema kuwa
akisema ndicho anachofanya.





No comments:
Post a Comment