masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, May 21, 2013

DIWANI ATAKA MGOGORO WA MACHINGA MASHINETATU UISHE


Diwani  wa kata  ya Miyomboni Kitanzia  Jescar Msambatavangu aliyekaa akizungumza na  wanahabari leo katika ofisi  za Klabu  ya waandishi wa habari Mkoa  wa Iring.



DIWANI wa Kata ya Miyomboni – Kitanzini Jescar Msambatavangu (CCM) amesema suala la wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wanaofanyia biashara zao Mashinetatu katika Manispaa ya Iringa linazungumzika.

Amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC).

Amesema bado kuna haja ya kukaa mezani kwa ajili ya kufanya majadiliano ili kulimaliza suala la machinga  ili waendelee kufanya biashara zao kwa uhuru.

Amesema japo kuwa kuna haja ya kukaa mezani bado kuna ugumu wa machinga kuendelea kufanyia biashara barabarani kutona na ongezeko la matumizi ya barabara na kkwa ustawi wa jamii.

“Kuna hali ya ugumu sana kwa machinga kuendelea kufanyia biashara zao mashinetatu kwa sababu ni barabara ambayo ongezeko la matumizi limekuwa kubwa” amesema.

Msambatavangu ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa amesema kuendelea kuwaacha machinga barabarani siyo vyema kwa usalama wa maisha yao na watu mbalimbali.

Amewataka wananchi kutoa mtizamo wa kisiasa kuwa mashinetatu kunafanyika kisiasa kwa kuwa bado kuna uhitaji wa matumizi ya barabara kwa kazi zingine.
 
“Tunachoangalia siyo maopato tu bali ni ustawi wa watu na maisha ya watu; nimezunguka maeneo yote ya Manispaa na kuona Mlandege kuwa kuna uafadhali ndiyo maana tunawaambia waende kufanyia biashara zao huko” amesema.

Alisema kutokana na uhaba wa barabara ndani ya Manispaa unaotokana na ongezeko la matumizi mbalimbali, barabara zinaendelea kujengwa ambapo zinafanyika jitihada za kukarabati barabara zinazounganisha mitaa ili kufungua upitikaji wa magari yanayoweza kusababisha msongamano.

No comments:

Post a Comment