| Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete anatarajia kuweka jiwe la msingi
katika ujenzi wa barabara ya Iringa -Dodoma kesho
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake leo Mkuu wa Mkoa
wa Iringa Dkt Christine Ishengoma amesema Rais Kikwete ataweka jiwe
la Msingi upande wa Iringa kesho (Mei 22 Mwaka huu) majira ya saa 3 asubuhi
katika eneo la Migoli na baada ya hapo mchana ataweka jiwe la
Msingi katika eneo la Fufu Escepment upande wa Dodoma.
Dkt Ishengoma amewataka
wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili
waweze kushuhudia uwekwaji wa jiwe hilo.
Pia amesema ujenzi wa barabara
hiyo utarahisisha usafiri wa mikoa ya Kusini na
Kaskazini mwa Tanzania
ambao ulikuwa mgumu na kuwafanya wasafiri kutumia gharama kubwa.
Hata hivyo amesema kuwa
ujenzi wa barabara hiyo umegawanyika katika maeneo matatu
ambayo kwa upande wa Iringa imegawanyika katika sehemu mbili
ikiwemo ya Iringa - Migoli yenye urefu wa kilometa 95.2 na
Migolo na sehemu ya pili kutoka Fufu Escapement ikiwa na urefu wa
Kilometa 93.2 wakati kutoka Fufu Escapement - Dodoma
90 .9 wakati thamani ya ujenzi wa barabara
hiyo kwa upande wa Iringa katika maeneo hayo ni kiasi cha
shilingi bilioni 84.2 fedha hizo ni malipo ya makandarasi na upande
wa usimamizi wa Tanroad ni 14 bilioni na kufikisha jumla ya shilingi 88
bilioni.
Hata hivyo amesema
kuwa ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma unatarajiwa
kukamilika mwaka 2015 na kufungua milango ya kiuchumi katika
Mkoa wa Iringa na Mikoa ya kusini mwa Tanzania .
Akielezea kuhusu
uchakavu wa barabara ya Iringa - Dodoma eneo la Mshindo hadi Kihesa
Kilolo ambayo pia ni barabara iliyopo katika mpango wa ujenzi huo, Ishengoma
amesema amemshauri meneja wa wakala wa barabara Mkoa
wa Iringa kuanza kuziba mashimo hayo wakati huu ambao bado ujenzi
huo kuanza katika eneo hilo.
Ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma utagharimu jumla ya 222 bilioni
No comments:
Post a Comment