| Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli aliwahutubia wakazi wa Migoli wakati wa uzinduzi wa barabara ya Iringa - Dodoma hii leo. |
| Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Migoli wakati wa uzinduzi wa barabara ya Iringa - Dodoma hii leo. |
RAIS
Jakaya Kikwete amezindua ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma kwa kuweka jiwe
la msingi katika kijiji cha Migoli na kuwataka wananchi waendeleze ujenzi huo
kwa kuwa waaminifu wa kutunza vifaa vya ujenzi na barabara hiyo kwa ujumla.
Uzinduzi
huo ulifanyika leo katika kijiji hicho kilochopo katika Kata ya Migoli Wilaya
ya Ieinga vijijini Mkoa wa Iringa ambapo licha ya kuwataka wananchi kuwa
waamifu Kikwete amewataka kudumisha amani na upendo kwa kuheshimiana.
“Barabara
hii itunzwe, msiibe mafuta na vifuri vya mitambo, tumechelewa sana kuwekeza
katika barabara kwa hiyo tukiwa na mitandao ya barabara nyingi nchini
tutafungua milango ya uchumi na uchumi utaongezeka” amesema
Amewataka
wananchi kutotumia tofauti zao kwa kuliingiza taifa katika machafuko na badala
yake amewataka wachape kazi kwa juhudi na maarifa.
“Matukio
ya hivi karibuni ni ya kusikitisha sana na hayafurahishi hata kidogo. Watu wabaya
tusiwape nafasi kwa sababu watatuingiza katika migogoro mikubwa” amesema.
Wakati
huo huo, Waziri wa ujenzi John Magufuli amesema hatakawia kuwatimua wakandalasi
watakaozembea na kwenda kinyume na mkataba wa makubaliano.
Amesema
hakuna sababu zitakazotolewa juu ya kuchelewa kukamilisha barabara hiyo kwa
kuwa tayari wakandalazi hao wamekwisha kulipwa fenda za kufanyia kazi.
“Wakandalasi
wameshalipwa fedha kwa ajili ya kujengea barabara hii kwa hiyo hakuna
kisingizio. Siwatanii wazembee nitawatimua” amesema Magufuli.
Amesema
tangu dunia iumbwe hakuna aliyefikiri barabara ya Iringa – Dodoma kama
itajengwa lakini umefika wakati ambao inalazimika kujengwa kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Katika
ujenzi wa barabara hiyo ambao utagharimu shilingi 232.2 bilioni, amesema hadi
sasa umekamilika kwa asilimia hamsini na tatu (53%) ambapo asilimia arobani na
saba (47%) unatarajiwa kukamilika kwa wakati.
Ujenzi
wa barabara hiyo umegawanyika katika maeneo matatu ambayo kwa upande wa
Iringa imegawanyika katika sehemu mbili ikiwemo ya Iringa -
Migoli yenye urefu wa kilometa 95.2 na Migoli, sehemu ya pili
ni Migoli – Fufu Escapement ikiwa na urefu wa Kilometa
93.2 na sehemu ya tatu kutoka Fufu
Escapement - Dodoma 90 .9.
Barabara
hiyo inajengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Japan, Benki ya Afrika (Africa Development
Bank (ADB)) pamoja na serikali ya Tanzania ambapo serikali ya Tanzania inatoa
fedha karibu asilimia sitini (60%).
Kwa
upande wake Mhandisi Mkuu wa barabara (Tanroad) alisema barabara hiyo inatakiwa
kukamilika kwa muda wa miezi 35 ambayo ni takribani miaka 3.
No comments:
Post a Comment