| Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita |
MKUU wa Wilaya ya Kilolo Gerald
Guninita amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuwatumia wataalam wa misitu katika
uvunaji wa misitu yao
ili kulinda mazingira.
Ameyasema haya ofisini kwake
katika mahojiano maalum na mtando huu juu ya ushiriki wa kuhifadhi mazingira.
Guninita amesema licha ya kuwa
kila mtu ana haki ya kuvuna msitu wake kwa matumizi mbalimbali, kuna haja kubwa
ya kuwatumia wataalam wa misitu ili kupata ushauri jinsi ya uvunaji na miti
inayopaswa kuvuna.
Amesema japokuwa kila mtu ana
msitu wake, si kila mti unatakiwa kuvunwa na kuna kiwango cha ukomavu wa mti
unaopaswa kuvunwa.
“Kwanza niwashukuru sana wale wote ambao
wamepanda miti kwa sababu hiyo ndiyo kampeni ya utunzaji mazingira
tunayoihamasisha ndani ya wilaya yetu. Upandaji wa miti uwe endelevu. Lakini ninawaomba
wananchi waelewe kuwa, tunakubali kuwa msitu alioupanda ni mali yake
lakini anapotaka kuvuna kwa matumii mbalimbali, awasiliane na wataalam wetu wa
misitu ili waweze kumshauri namna ya uvunaji na miti gani inapaswa kuvunwa”
amesema Guninita.
Amesema ukiukwaji wa uvunaji wa
miti katika maeneo mbalimbali utachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa
unachangia maingir kuharibika na kupoteza sura.
“Kuwa na miti ni yambo muhimu kwa
kuwa mazingira yetu yanakuwa safi
na salama, hewa inakuwa nzuri na ongezeko la joto linapungua lakini miti na
misitu kwa ujumla inapokatwa bila utaratibu, hali ya hewa inaharibika” amesema.
Amesema wapo baadhi ya watu ambao
wamekwishapata onyo kama fundisho kwa kukiuka
utaratibu wa kuvuna miti na kusema endapo atajitokeza mtu anavuna kinyume cha
utaratibu atachukuliwa hatua kali a kisheria.
“Tunapenda watu wetu wawee
kutumia mali zao kwa ajili
ya kuendesha maisha yao lakini mali hizo pia
zinatakiwa kutumika kwa autaratibu. Kinyume na hapo hatua za kisheria inafuata
japo kuwa ni mali
yake” amesema.
Wilaya ya Kilolo imepanda miti
aidi ya ekari 10 kwa ajili ya kuendeleza uhifadhi wa mazingira na kwamba
mkakati huo unaendelea.
No comments:
Post a Comment