![]() |
| Mwanamke wa Bangladesh anusurika baada ya siku kumi na saba |
Waokoaji nchini Bangladesh wamemuokoa mwanamke mmoja kutoka kwa vifusi vya jengo lililoporomoka yapata siku 17 zilizopita.
Miujiza
Waokoaji hao wametaja hilo kama miujiza. Ikiwa zimepita zaidi ya wiki mbili tangu jengo hilo la orofa nane kuporomoka, walikuwa tayari wameshaanza kukata tamaa ya kumpata mtu mwengine yoyote hai.Lakini wanajeshi walipokuwa wanazoa zoa vifusi katika orofa ya chini walisikia sauti ikiita. Walitumia vifaa vyao maalum ambavyo vilionyesha dalili za uhai chini ya vifusi.
Mwanamke huyo aliitana akitaja jina lake kama Reshma. Baada ya juhudi za pamoja waokoaji pamoja na wanajeshi walifanikiwa kumtoa mwanamke huyo alikonaswa na kumkimbiza hospitalini.
![]() |
| waokoaji walianza kupoteza matumaini |
Jamii ya kimataifa
Ajali hiyo ya Bangladesh imesababisha mataifa mengine hasa ya magharibi kama vile Uingereza kutilia shaka bidhaa za kutoka nchini Bangladesh kwa namna zinavyotengenezwa na uwezekano wa kunyanyaswa wafanyikazi.
Chanzo: bbc swahili


No comments:
Post a Comment