![]() |
| Huyu ndie mtuhumiwa wa mauawaji ya Mwangosi (kulia) |
WAZIRI wa sheria na katiba Mathias Chikawe awadanganya watanzania kuhusu upelelezi wa kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa leo mahakamani na mahakama hiyo kuelezwa kuwa upelelezi bado kukamilika.
Waziri Chikawe alilidanganya bunge hivi karibuni wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu ucheleweshaji wa usikilizaji wa kesi hiyo ya mtuhumiwa huyo wa mauwaji ya Mwangosi , askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni ambapo waziri alisema kuwa upelelezi wake umekamilika.
Katika hali iliyowashtua wengi leo mahakamani hapo ni baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa kwa mara nyingine mahakamani hapo na wakili upande wa jamhuri Adolph Maganda kuomba mahakama hiyo kutoa tarehe nyingine ya kesi hiyo kutajwa kutokana na upelelezi wake kutokamilika.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo ghafla leo baada ya kumbukumbu za awali kuonyesha kuwa kesi hiyo ingetajwa May 9 ila jana alifikishwa mbele hakimu mkazi, mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Juma Hasan kiasi cha hakimu huyo kulazimika kumuuliza mtuhumiwa huyo kama ni yeye kweli ama la.
Baada ya kesi hiyo namba 1/2012 ya mauwaji inayomkabili askari huyo wa FFU kutajwa mbele ya mahakama hiyo kwa mtuhumiwa kuitwa kizimbani hakimu huyo alionyesha shaka na kulazimika kumhoji mtuhumiwa kwa mshangao kama ni kweli jina hilo ni lake na yeye ndio mhusika ama vipi.
“Eti ni kweli wewe ndio mwenye jina hili na mhusika na kesi hii iliyotajwa?" alihoji hakimu huyo na mtuhumiwa huyo kuthibitisha kwa sauti kuwa ni kweli mheshimiwa hakimu.
Hata hivyo wakili wa serikali Adolph Maganda aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado kukamilika.
Kesi hiyo itatajwa tena May 22 mwaka huu na mtuhumumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi hiyo kukosa dhamana kisheria.

No comments:
Post a Comment