| Barabara hii haijamaliza hata miaka 2 tangu kujengwa. |
Hii ni barabara ambayo hata miaka 2 haijapita tangu
itengenezwe lakini iko katika hali hii.
Hii ni barabara inayoanzia Kihesa sokoni kuelekea Chuo Kikuu
cha Tumaini ambayo haijafunga hata miaka miwili tangu ilipotengenezwa.
Kuna haja ya kupitia upya sifa za makandarasi wetu wanaopewa
kazi hizo ili kuepukana na matatizo kama haya.
Pia nafikiri kuna haja ya makandarasi wetu kujifunza kwa
wenzetu waliobobea katika masuala ya ujenzi wa barabara ili kuepusha matumizi
mengi ya ujenzi wa barabara usio wa lazima kwa kuwa baada ya muda mfupi
zinakuwa zimebomoka.
Hivi sasa karibu barabara zote za Manispaa ya Iringa
hazitamaniki kutokana na kuharibika vibaya.
No comments:
Post a Comment