masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, April 13, 2013

WAFANYABIASHARA WADOGO WATANGAZA VITA NA MGAMBO

Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa akiwahutubia wakazi wa Mwangata katika mkutano wa kiserikali aliouandaa kwa ajili ya kuongea na wananchi.

Mgunge Msigwa akimkabidhi kisemeo mfanyabiashara Michael Raphael ili aweze kutoa kero zake.


WAFANYABIASHARA wadogo maarufu kwa jina la machinga katika Manispaa ya Iringa wametangaza vita na Mgambo wa mji wanaowafukuza na kuwanyang’anya mali zao.

Haya yamezungumzwa na Michael Raphael kwa niaba ya wafanyabishara wenzake mbele ya Mbungu wa Iringa mjini Peter Msigwa (CHADEMA) katika mkutano wa kiserikali ulioandali wan a mbunge huyo na kufanyika katika viwanja vya Mwangata juzi.

Alisema kumekuwa na tabia ya mgambo kuwafukuza wafanya biashara hao pamoja na kuwanyang’anya mali zao na kupeleka kwa Mkurugenzi wa Manispaa kwa lengo la kulipia shilingi 50 elfu jambo ambalo limekuwa likiwakwambisha kukabiliana na hali ngumu ya maisha iliypo sasa.

“Mbunge wetu tunaomba msaada kwa hili, mgambo wamekuwa wakitunyanyasa sana. Wanatufukuza na kutunyang’anya mitaji yetu. Sisi tuende wapi na tufanye shughuli gani kwa ajili ya kuendesha maisha yetu? Tumekopa kwa ajili ya kufanya biashara ndogo lakini hizo hizo wanatunyang’anya, tufanye nini? Sasa tunatamka mbele yako kuwa kuanzia leo, kama kuna mtu hapa ndugu yake ni mgambo akamwambie kuwa tunatii mamlaka tu ila hawawezi kutushinda kwa lolote. Tunatangaza vita dhidi yao kuanzia sasa. Mgambo ye yote atakayemsumbua mfanyabiashara tunaye kwa namna yo yote ile” alisema.

Kwa upande wake Mbunge Msigwa alisema hayupo tayari kuona wafanya biashara wananyanyasika na mgambo na kuwataka wafanyabiashara hao kuuungana na kuwa kitu kimoja ili kuhakikisha manyanyaso hayapo.

“Nawaunga mkono, sipo tayari kuona mnanyanyaswa na mgambo. Popote mtakapoona mnanyanyasika nipeni taarifa. Nipo tayari kupigwa mimi kuliko manyanyaso mnayoyapata kwa mgambo” alisema Msigwa.

Awali Agnes Kilamulilo mfanyabiashara wa nyanya alisema mgambo wamekuwa na tabia ya kuomba rushwa ili kuwaacha kuendelea kufanya biashara na wakati mwingine akina mama wamekuwa wakiomba rushwa ya ngono na wanapokataa wamekuwa wakinyang’anywa mali zao.

Katika mkutano huo, wananchi wamemtaka Mbunge Msigwa kuwa mkorofi zaidi bungeni kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwa wamekuwa wakishuhudia vitendo vya unyanyasaji na uonezi vinavyofanywa na meza ya spika wa bunge.

Wamesema awe mkali kuliko kawaida kwa kuwa nchi hii imefikia mahali usipotumia ukali na maandamano upewa haki si rahisi.

Katika hatua nyingine Msigwa amemtaka kamanda wa polisi Michael Kamuhanda anapomkamata mhalifu aache tabia ya kuhusisha uhalifu na chama kwani hiyo siyo kazi yake.

“Natuma taarifa hii hata nyie polisi mliopo mkamwambie bosi wenu Kamuhanda kuwa anapomkamata mhalifu aache tabia ya kumhusisha na chama. Huo ni uhuni na utovu wa nidhamu hususani ukiukaji wa maadili ya kazi. Hizo tunajua kuwa ni mbinu za chama cha mapinduzi kumtumia Kamuhanda kukichafua Chadema. Asifikiri tumesahau yale ya Nyololo bado wananchi wanayakumbuka. Kamuhanda aueleze umma kuwa yeye ni kada wa CCM ili ijulikane moja” alisema.

No comments:

Post a Comment