masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, April 11, 2013

MBUNGE MSIGWA AMVAA KIKWETE

Baadhi ya wananchi waliofika kumsikiliza Mbunge wao Peter Msigwa.
Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwagonjo Ipogolo katika Manispaa ya Iringa jana jioni.



MBUNGE wa Iringa Mjini Peter Msigwa (CHADEMA) amesema Rais Kikwete ameshindwa kuwahudumia wazee wastaafu na kubaki akitoa malalamiko na kuaminisha wananchi kuwa yeye ni kiongozi bora.



Mch. Msigwa aliyazungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwagongo Ipogolo katika Manispaa ya Iringa alipokuwa akipokea kero na maoni kutoaka kwa wananchi.



Alisema serikali ya Kikwete imebaki kuwa kichekesho kwa kwa mataifa mengine kwa kushindwa kutoa huduma bora na kugeuza nchi kuwa ya kihuni kutokana na viongozi wenye fikra mfu aliowateua.



“Kipindi cha Mkapa wazee wastaafu walikumbukwa kwa kiasi fualani, lakini katika utawala wa Kiwete hana habari kabisa kuwa nchi hii ina wazee na watu wanaolipa kodi ambazo watu wake wenye fikra fupi aliowateua wanazitafuna kila kukicha” alisema.



Alisema kutokana na ufupi wa mawazo ya viongozi, haa usalama wa taifa umechoka kwa kuwa hawawezi kufanya kazi kwa uhuru kwa sababu ya kiongozi wao mwenyewe kuruhuru ujangili na matukio yasiyo ya lazima kwa maslahi yake mwenyewe.



“Usalama wa taifa umechoka. Huwezi kusema una usalama wa taifa wakati ndege za kijangili zinatua nchini na kubeba Twiga na Vifaru huku wakiona na kubaki waking’aa macho tu” alisema.



Alisema serikali ya Mkoloni iliwaheshimu wamasai na kuwaachia ardhi kwa ajili ya kufuga wanyama kwa ajili ya kuendesha maisha yao lakini cha kushangaza serikali ya CCM haiwathamini tena watu kupitia ardhi na badala yake wanaofaidi ardhi ni wageni.



“Mmasai alifuarahia mapori wakati wa serikali ya mkoloni. Tangu serikali ya CCM kuingia madarakani mmasai huyuhuyu amekuwa akinyanyasika maisha yake yote kwa sababu serikali ya CCM inamfukuza ili ardhi hiyo wampatie muarabu na watu wengine. Ukiona jirani yako anaonewa ujue hata wewe unaonewa” alisema.



Ameeleza kuwa kwa ujumla serikali ya chama cha mapinduzi inamatumizi mengi kuliko uwezo wa watanzania ndiyo maana mikopo ni mingi kuliko kipato.



Katika hatua nyingine Msigwa alisema matatizo ya wananchi yanatokana na kuwa na viongozi wapuuzi wasiokuwa na huruma kwa watu wao na kutumia madaraka yao kwa vitisho.



“Kuanzia leo, namtaka Mkurugenzi wa Manispaa kuacha tabia ya kuwakusanya wafanyakazi wa umma na kuwataka waendende kumsikiliza mwanachama wa CCM. Huo ni ukiukwaji wa sheria za kazi na maadili ya utumishi. Mkurugenzi asifikiri hatujui, tunajua vizuri” alisema.



Alisema badala ya Mkurugenzi huyo kukaa na kupanga mikakati ya kutatua matatizo ya wananchi amekuwa kikwazo kwa walipakodi kutuma mgambo kuwanyanyasa wananchi na kupiga alama ya X kwenye nyumba zao.



“Na kuanzia sasa, sipo tayari kuona mgambo wanawanyanyasa watu barabarani eti wanafanyafanya biashara kinyume. Kama wanafanya biashara kinyume mbona ushuru wanapokea? Sipo tayari kuona watu wanabomolewa nyumba zao wakati kodi za majengo hayo wanazipokea. Wananchi, unganeni pamoja na muhakikishe mtu yeyote asiwanyanyase. Lakini hata hivyo hakikisheni mfumo wa viongozi tulionao unabadilishwa vinginevyo tutaendelea kunyanyaswa maisha yetu yote” alisema.

No comments:

Post a Comment