![]() |
| Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Theresia Mahongo. |
MKURUGENZI wa Manispaa ya Iringa
Theresia Mahongo amelalamikiwa kufanya kikao na wafanyakazi kuwatisha kuwa
wasipokipenda Chama cha Mapinduzi (CCM) watafukuzwa kazi.
Katika kikao chake alichokifanya
na wafanyakazi hao katika ukumbi wa
Wellfair Aprili 4 majira ya mchana,
Mahongo alisema kuwa ni marufuku kushabikia vyama vya upinzni na iwapo
itabainika kuwa kuna anaeshabikia CCM atafukuzwa kazi. Tanzania Daima
limedokezwa.
Imeelezwa kuwa mkutano huo ni
utekelezaji wa mikakati iliyowekwa kwa ajili ya kuwabana wale wanaoshabikia
vyma vya upinzani kote nchini ikiwa utekelezaji huounaanzia kwa wafanyakazi
serikalini.
“Tuliambiwa kuwa kutakuwa na
kikao katika ukumbi wa Wellfair ambapo baada ya kufika katika kikao hicho
agenda iliyoongelewa ni moja tu kututisha wafanyakazi kuwa atakayechabikia
vyama vya upinzani anafukuzwa kazi. Hii siyo demokrasia kabisa hata uhuru haupo
sasa kwa sababu watu tunabanwa kiasi cha kutokuwa na uhuru wa maamuzi” kilisema
chanzo chetu.
Kwamba hali ya ufanyaji kazi
inakuwa ngumu kwa kuwa watu wanafanya kazi kwa hofu hata kuongea na watu
inakuwa ngumu hususani wanaojulikana kuwa ni wa upinzani wanapofika ofisini na
shida zao imekuwa ni vigumu kuwahudumia ipasavyo kwa wakiogopa kuwa watahisiwa
kuwa wanajadili siasa.
“Tunashindwa kujua mpango wao ni
nini kutumia vitisho kama hivi. Tunajiuliza,
kwani wameshtuka nini kutumia njia ya vitisho wakati huko nyuma haikuwa hivyo?
Ama kweli mnyonge ni mnyonge tu” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa kwa
hatua waliyofikia sasa, lawama za kila aina zitakuwa nyingi kutoka kwa wateja
kwa kuwa utendaji wa kazi utakuwa ni wa hofu kuwa ni wa kisiasa.
“Tulipofikia na tunakokwenda ni
kugumu kwa sababu hata kuwahudumia watu itakuwa ni vigumu jambp litakalosababisha
lawama nyingi kutoka kwa wateja wetu juu ya uwajibikaji wetu kwa sababu
tutakuwa tunaogopa kuwa ni akina nani tunawahudumia” kilisema chanzo hicho.
Mkurugenzi huyo alipotafutwa mara
kadhaa kwa njia ya simu, simu imekuwa ikiita bila kupokelewa mpaka pale ilipobadilishwa
simu nyingine ndipo ilipo alipopoikea simu.
Alipotakiwa kutolea maelezo juu
ya hilo alisema
hajui lolote kwa kuwa ofisi alimuachia mtu yeye akiwa safarini.
“Mimi sijui lolote kwa sababu
nilikuwa safarini na ofisi nilimwachia mtu hata niliporudi hakuniambia
chochote” alisema Mahongo.
Hata hivyo alisema sheria na
taratibu za serikali zinajulikana kwa hiyo kitakachomfukuza mtu kazi ni
taratibu na sheria hizo.
“Lakini hata kama
sikuwepo, mtu atafukuzwa tu bila sababu? Taratibu na sheria zinajulikana kwa
hiyo si mimi nitakayemfukuza bali ni taratibu tu. Ila nikwambie tu kuwa kwa
ujumla sijui lolote” alisema Mkurugenzi Mahongo.
Katika hatua nyungine, mratibu wa
baraza la vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Iringa Aidan
Salehe amesema kitendo cha kutumia vitisho kwa wafanyakazi ni ukiukaji wa
katiba na sheria za nchi.
“Tunamshauri Mkurugenzi ajenge
barabara za Manispaa zilizoharibika badala ya kuitisha vikao vya kuwatisha
wafanyakazi. Ingependeza kama anaitisha vikao vya kujenga barabara na kuboresha
maisha ya wanairinga badala ya kutumia madaraka yake kwa vitisho” alisema.


No comments:
Post a Comment