masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, April 10, 2013

KAMUHANDA AKEMEWA NA VIJANA IRINGA

Mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na Maendeleo BAVICHA akitoa tamko la kumukemea Kamuhanda juu ya taarifa zake kwa vyombo vya habari.

KAMANDA wa Polisi Mkowa wa Iringa Michael Kamuhanda ametakiwa kuacha mara moja tabia ya kutumia madaraka vibaya kwa kuwazushia wananchi ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka yake kisiasa tofauti na maadili ya kazi yake.

Haya yamezungumzwa leo na Mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chama cha Demkokrasia na Maendeo (BAVICHA) Mkoa wa Iringa Joseph Nzala Lyata akikanusha taarifa ya Kamuhanda juu ya Athanas Mongo (mtuhumiwa wa ujambazi) kuwa ni Kamanda wa BAVICHA.

Amesema BAVICHA Mkoa wa Iringa waesikitishwa na kitendo cha Kamuhanda kujivika jukumu la kuwapachika raia vyeo ambavyo haviko kwenye utaratibu wa CHADEMA wala BAVICHA kwa kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kujaribu kukipaka matope Chadema.

“Tunapenda kuufahamisha umma kuwa zilizotolewa na Kamuhanda, RPC wa Iringa na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Athanas Mongo (mtuhumiwa wa ujambazi) ni kamanda wa vijana wa CHADEMA Mkoa wa Iringa ni uongo na uzushi wenye hila za makusudi za kujaribu kuharibu taswira ya BAVICHA na CHADEMA kwa umma” amesema.

Amesema Mongo si Kamanda wa Bavicha Mkoa wa Iringa na wala muongozo wa Mabaraza ya Chama unaosimamia mabaraza yote likiwemo Bavicha kwa upande mmoja na Katiba ya Chadema kwa upande mwingine haina wala haitambui cheo ambacho RPC Kamuhanda kamvisha Mongo.

“Tunavyojua sisi hicho ni cheo kinachotumiaka na chama cha mapinduzi (CCM). Sasa labda RPC Kamuhanda ni mzoefu wa kukariri vyeo vya CCM. Yeye anajua hilo” alisema na kwamba “Mongo ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA na asiyekuwa na cheo chochote ndani ya BAVICHA wala CHADEMA. Ni mtanzania mwenye haki ya kuwa mwnachama wa chama chochote cha siasa. Kutuhumiwa kwake kwa masuala ya uhalifu hakupaswi wala hakuwezi kuhusishwa na Chadema wala Bavicha” amesema.

Amesema Bavicha wanamuonya Kamuhanda kuacha mara moja tabia ya kukurupuka na kutokuwa makini katika utendaji kazi kiasi cha Bavicha ili tu kukidhi haja yake ya kuipaka matope CHADEMA baada ya kushindwa hila hizo kwenye tukio la mauaji ya mwandishi wa habari, marehemu Daudi Mwangosi kule Nyololo.

“Bila shaka ni ukurupukaji na kukosa umakini kama huu, ndiyo uliosababisha RPC Kamuhanda akakiuka misingi ya utawala bora kama ilivyoelezwa na ripoti ya uchunguzi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala juu ya mauaji ya Mwangosi” amesema.

Amesema kutokana na mauaji ya mwandishi wa habari, Kamuhanda anajaribu kufanya kila mbinu kutumia nafasi yake kukichafua Chadema huku akijua kuwa anakiuka utaratibu na anakwenda kinyume na utawala bora kwa kujisafisha mauaji yaliyofanyika.

“Uchunguzi wa THUB ambacho ni chombo cha serikali chenye majukumu ya kikatiba na kisheria kuhusu masuala ya haki za binadamu ulibaini kuwa RPC Kamuhanda mnamo 02.09.2012 alikiuka sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11 (a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi na kutoa amri ya kuzyia shughuli za CHADEMA wakati yeye hakuwa “Officer In-charge” wa polisi wa eneo husika. Kwa maana hiyo aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri hiyo. Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora” amesema.

Amesema kutokana na uchunguzi huo, unaonesha uendaji mbovu wa Kamuhanda, RPC pamoja na polisi wenzake walioshiriki katika tukio la Nyololo kumuua mwandishi wa habari.

“Baada ya kufanya mauaji hayo Kamuhanda na wenzake walianza kufanya propaganda za kuipaka matope CHADEMA ili kuwanusuru wao, alipaswa kuwa amejiuzulu au amefukuzwa kazi na kushtakiwa mahakamani kutokana na tukio hilo la mauaji ya Mwangosi kama ambavyo Chadema imeshauri mara kadhaa, ikiwemo kuandika barua kwa Rais Jakaya Kikwete” amesema.

Kamuhanda alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) mkoa wa Iringa Athanas Mongo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ujambazi.

Kamuhanda alisema kiongozi huyo wa Bavicha na wenzake wanatuhumiwa kufanya ujambazi uliotokea Machi 15 mwaka huu kwa kutumia silaha.

No comments:

Post a Comment