masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, April 22, 2013

WACHINA WANUSURIKA KICHAPO KWA ABIRIA MTERA

Barabara ikiendelea kuchimbuliwahuku magari ya abiria yakiwa yamesismama kukosa sehemu ya kupita.

Abiria walioshuka kwenye basi na kuamua kuwasogelea wachina waliokuwa wakiendelea kufanya kazi bila kuacha barabara ya kupita magari na kuanza kupiga mayowe.

Mmoja wa abiria akimkaripia mchina kumtaka kuacha barabara ili magari yapite kwanza.

WACHINA wanaojenga barabara ya Iringa - Dodoma wamenusurika kuchapwa na abiria walilokuwa wakisafiri na basi la Upendo kutoka Dodoma kwenda Iringa.

Kizaa zaa hicho kilikujaa baada ya wachina hao kuona magari yanakuja na kuanza kuchimbua barabara karibu na geti la bwawa la mtera bila kuacha nafasi ya kupita magari mengine.

Abiria walipandisha hasira baada ya saa zima kupita bila kuona dalili za kupita mahali hapo huku wachina hao wakuendelea kuelekeza wafanyakazi wao sehemu zingine za kuchimbua.

Wakati wakiendelea na maelekezo kwa wafanyakazi wao, abiria waliamua kutoka kwenye gari na kuwashambulia wachina hao wakisema acheni mambo yenu ya makusudi na sisi tuna haki ya kusafiri.

huku mayowe yakizidi kuwaandama wachina hao bila kuelewana lugha baadhi ya abiria waliamua kuokota mawe na kuwaambia wachina wakisema upepo utachafuka.

"Patachimbika hapa sasa hivi kwa mabo yenu mnayoyafanya. Saa zima tumesimama hapa mnajifanya kama hamtuoni. Mtabeba mawe haya sasa hivi. Fanyeni haraka sisi tupite ndiyo muendelee na kazi zenu" zilizikika sauti hizo.

Baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo maeneo hayo waliwasogelea wachina hao na kuongea nao ndipo walipoamua kuingia wenyewe kwenye mashine zao za barabara na kuamua kutoa udongo sehemu kidogo ili kuruhusu magari yapite.

No comments:

Post a Comment